TFF amkeni, siasa chafu zaja michezoni

TFF amkeni, siasa chafu zaja michezoni

Shakidinkili

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
458
Reaction score
174
Mpira wa miguu ni moja ya michezo inayopendwa sana duniani, hivyo mpira wa miguu una umaarufu mkubwa sana.

Mh. Esther Bulaya, mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara kwa tiketi ya CCM, amejitoa kimasomaso kwa kufadhili mashindano ya mpira wa miguu wilayani Bunda. Mashindano haya yanashirikisha vijana wengi kutoka wilaya hiyo na manufaa yake yameonekana ikiwa ni pamoja na.

1. Kufahamiana na kuzoeana zaisi kwa vijana wilayani Bunda.
2. Kuzalisha ajira ya muda kwa vijana wilayani Bunda.
3.Kuimarisha mshikamano miongoni mwa vijana.
4. Kuibua vipaji vijijini na hatimaye kupata Wanamichezo wazuri na bora nchini.

Katika hatua isiyo ya kawaida na ya kushangaza, Mkuu wa Wilaya ya Bunda ameyapiga marufuku mashindano hayo kwa kisingizio ATI YANAENDESHWA NA MWANASIASA BADALA YA TFF. Sijui ametumia vigezo gani hadi kufikia uamuzi huu, lakini tumeshuhudia sehemu mbali mbali hapa nchini zikiendesha mashindano yanayofanana na haya na kwa ufadhilli unaofanana na huu bila matatizo kama vile KOMBE LA SHIGONGO huko Mwanza.

Nikizingatia sababu aliyoitoa kuwa yanaendeshwa na Mwanasiasa, inaonyesha wazi uamuzi huu ni wa kisiasa vile vile. Ina maana kama Mh. Esther Bulaya angekuwa sio mwanasiasa, mashindano haya yangeendelea pasipo vikwazo. Ninashawishika kuamini kuwa Mh. DC ametumiwa tu na wanasiasa wengine, mdomo wake umetumiwa vibaya. Tunajua Ma DC ni makada wa CCM na Mh. Esther Bulaya ni mwana CCM, aidha haya ndio matunda ya KURA YA WAZI NA KURA YA SIRI iliyowagawa CCM mjengoni.

Nani asiyejua msimamo wa Mh. Esther Bulaya uliokinzana na msimamo wa chama chake. Huku ni kushung'ulikiana kisiasa au ni maelekezo ya wale wanaodhani wana hati miliki za majimbo ya uchaguzi, uchaguzi mkuu unakaribia hivyo hofu na kiwewe vimetanda kuwa Mh.Esther anapata umaarufu jimboni kupitia mashindano haya na atakuwa tishio kwa hati miliki zao endapo atasimama kugombea jimboni.

Hata kama mashindano haya yanakumbwa na kasoro ndogo ndogo bado mimi ninaamini kasoro hizo zinarekebeshika kupitia Shirikisho la mpira wa miguu wilayani Bunda kwa kushirikiana na Mfadhili wao, suluhisho sio kuyapiga marufuku mashindano haya. Marufuku ni mtazamo hasi.

TFF amkeni, toeni kauli na msimamo wenu mapema, vinginevyo sumu imemwagwa Bunda inaweza kuenezwa nchi nzima kwa matakwa ya KISIASA.
 
Mpira wa miguu ni moja ya michezo inayopendwa sana duniani, hivyo mpira wa miguu una umaarufu mkubwa sana.
Mh. Esther Bulaya, mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara kwa tiketi ya CCM, amejitoa kimasomaso kwa kufadhili mashindano ya mpira wa miguu wilayani Bunda. Mashindano haya yanashirikisha vijana wengi kutoka wilaya hiyo na manufaa yake yameonekana ikiwa ni pamoja na.
1. Kufahamiana na kuzoeana zaisi kwa vijana wilayani Bunda.
2. Kuzalisha ajira ya muda kwa vijana wilayani Bunda.
3.Kuimarisha mshikamano miongoni mwa vijana.
4. Kuibua vipaji vijijini na hatimaye kupata Wanamichezo wazuri na bora nchini.
Katika hatua isiyo ya kawaida na ya kushangaza, Mkuu wa Wilaya ya Bunda ameyapiga marufuku mashindano hayo kwa kisingizio ATI YANAENDESHWA NA MWANASIASA BADALA YA TFF. Sijui ametumia vigezo gani hadi kufikia uamuzi huu, lakini tumeshuhudia sehemu mbali mbali hapa nchini zikiendesha mashindano yanayofanana na haya na kwa ufadhilli unaofanana na huu bila matatizo kama vile KOMBE LA SHIGONGO huko Mwanza. Nikizingatia sababu aliyoitoa kuwa yanaendeshwa na Mwanasiasa, inaonyesha wazi uamuzi huu ni wa kisiasa vile vile. Ina maana kama Mh. Esther Bulaya angekuwa sio mwanasiasa, mashindano haya yangeendelea pasipo vikwazo. Ninashawishika kuamini kuwa Mh. DC ametumiwa tu na wanasiasa wengine, mdomo wake umetumiwa vibaya. Tunajua Ma DC ni makada wa CCM na Mh. Esther Bulaya ni mwana CCM, aidha haya ndio matunda ya KURA YA WAZI NA KURA YA SIRI iliyowagawa CCM mjengoni. Nani asiyejua msimamo wa Mh. Esther Bulaya uliokinzana na msimamo wa chama chake. Huku ni kushung'ulikiana kisiasa au ni maelekezo ya wale wanaodhani wana hati miliki za majimbo ya uchaguzi, uchaguzi mkuu unakaribia hivyo hofu na kiwewe vimetanda kuwa Mh.Esther anapata umaarufu jimboni kupitia mashindano haya na atakuwa tishio kwa hati miliki zao endapo atasimama kugombea jimboni. Hata kama mashindano haya yanakumbwa na kasoro ndogo ndogo bado mimi ninaamini kasoro hizo zinarekebeshika kupitia Shirikisho la mpira wa miguu wilayani Bunda kwa kushirikiana na Mfadhili wao, suluhisho sio kuyapiga marufuku mashindano haya. Marufuku ni mtazamo hasi. TFF amkeni, toeni kauli na msimamo wenu mapema, vinginevyo sumu imemwagwa Bunda inaweza kuenezwa nchi nzima kwa matakwa ya KISIASA.

ahsante Shakidinkili.
thread yako imenishtua.
Ngoja nifuatilie.Kimsingi ni vigumu sana kuendesha mpira nchini mwetu bila ushirikiano wa viongozi wetu maana kupitia kwao tunapata mashindano mbali mbali kuazia ngazi ya kata,tarafa,wilaya na hata mikoa.Viongozi wetu ni wadau wakubwa sana wa mpira.
 
Last edited by a moderator:
Mleta maada una speculations kibao, kura ya wazi na siri, kuingilia hakimiliki, dc kutumiwa du ester bulaya anaishi wapi now?
 
wenyewe wamekusikia....lakini na wewe ni kama mwanasiasa vileee.
 
ahsante Shakidinkili.
thread yako imenishtua.
Ngoja nifuatilie.Kimsingi ni vigumu sana kuendesha mpira nchini mwetu bila ushirikiano wa viongozi wetu maana kupitia kwao tunapata mashindano mbali mbali kuazia ngazi ya kata,tarafa,wilaya na hata mikoa.Viongozi wetu ni wadau wakubwa sana wa mpira.
Kwako Ndugu J.Malinzi, Raisi wa TFF.Nimerudi tena hapa uwanjani mara tu baada ya kuona taarifa kwenye Runinga. Nimerurahishwa na hatua ya kuona mashindago ya mpira wa miguu wilayani Bunda yanayofadhiliwa na Mbunge Mh. Esther Bulaya yamerejeshwa. Mimi sio mkazi wa wilaya ya Bunda lakini kitendo kile kilinikera sana.Niaamini juhudi zako kama ulivyoahidi humu zimechangia kuondolewa kwa zuio hilo. Hongera sana. Zuio limebainika lilikuwa na mtazamo wa kisiasa zaidi pasipo kujali maslahi ya vijana wa Bunda. hawa wanasiasa wetu bwana, acha tu niishie hapa. Wish you all the best while perfoming your daily duties in the office.
 
Fainali zitakuwa tarehe 22/05/2014 karibu!
 
Back
Top Bottom