TFDA mnatuchanganya kuhusu Metakelfin | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFDA mnatuchanganya kuhusu Metakelfin

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MIGNON, Sep 7, 2010.

  1. M

    MIGNON JF-Expert Member

    #1
    Sep 7, 2010
    Joined: Nov 23, 2009
    Messages: 2,097
    Likes Received: 913
    Trophy Points: 280
    Ninasikiliza power breakfast ya Cloud FM na anayojiwa mtalaamu wa TFDA kuhusu matumizi ya Metakelfin na anaeleza ya kuwa batch zilizokuwa na hitilafu ziliondolewa na zinazo ingizwa sasa zina kiwango kinachotakiwa.Nahoji yafuatayo,
    -Ilishathibitishwa ya kuwa dawa za jamii ya SP hazina uwezo wa kutibu kwa kiwango kianchotakiwa na ndo maana dawa mseto ikaingizwa.
    -Mfumo uliopo wa matumizi ya SP ni katika kuwalinda wajawazito tu.
    Hivyo kuruhusu dawa hizi kuuzwa katika maduka ya kawaida kuna wa encourage watu kutumia dawa ambayo imeshaonyesah kwa kiwango kikubwa kushindwa kutibu malaria.
    Kwa kuwa uelewa wa watu wengi ni mdogo watakimbilia dawa ya kunywa mara moja kuliko Mseto ambayo unatakiwa ufuate msaa maalum kwa muda wa siku tatu.
    NAshauri SP zipatikane katika Clinic za waja wazito tu,otherwise tunahatarisha maisha ya watu kwani wengi wanaoanza na SP ikiwemo metakelfin wanachelewa kupata matibabu sahihi na kuna uwezekano wakafika hospitalini wakiwa wamezidiwa zaidi.
     
  2. KIWAVI

    KIWAVI JF-Expert Member

    #2
    Sep 7, 2010
    Joined: Jan 12, 2010
    Messages: 1,601
    Likes Received: 263
    Trophy Points: 180
    uko wrong! umeamua kujichanganya

    si lazma dawa ikiwa sio first line katika guideline basi isiuzwe kabisa.... ndio maana kuna recommended treatment of choice and alternative treatments

    rejea guidelines na medical infomration vipo hata mitandaoni

    Vipi kuhusu asprin, paracetamol, diclofenac etc?
     
  3. M

    MIGNON JF-Expert Member

    #3
    Sep 7, 2010
    Joined: Nov 23, 2009
    Messages: 2,097
    Likes Received: 913
    Trophy Points: 280
    Siamini kama nimejichanganya ila nakuomba upitie Malaria treament guidelines iliyotolewa na NMCP na uone nafasi ya SP.
    Pia tafakari na jiulize kwa nini iliondolewa,uwezo wa kutibu ulishuka kwa kiwango gani?Tafakari zaidi.
     
Loading...