TETESI ZA USAJILI ULAYA 9/1/2016

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,455
TETESI ZA SOKA ULAYA- JUMAMOSI 09.01.2015
Real Madrid wanamtaka beki wa kati wa Everton, John Stones, 21, kufuatia ushauri wa kocha waliyemtimua Rafael Benitez (Daily Mail), Manchester United wamemuulizia kocha wa Paris St-Gremain, Laurent Blanc, kama ataweza kujiunga nao sasa hivi au mwisho wa msimu (Le10),
meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameweka jina la mshambuliaji wa Watford, Odion Ighalo, 26, kwenye orodha ya wachezaji anaowataka mwisho wa msimu huu (Daily Mirror),
meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amezungumza na wakala wa Mario Balotelli, 25, kutaka kumrejesha Anfield kutoka AC Milan (Tuttomercatoweb),
West Brom wanataka kumsajili mshambuliaji Gabriel Agbonlahor, 29, kutoka Aston Villa kabla ya mwisho wa mwezi huu (Sun),
kiungo wa Bayern Munich, Mario Gotze, 23, amesema hatma yake Ujerumani iko katika ati ati, na amekuwa akimsifia meneja wa Liverpool Jurgen Klopp, ambaye alikuwa naye Borussia Dortmund (Bild),
Real Madrid wanafikiria kupanda dau la zaidi ya pauni milioni 100 kumtaka Paul Pogba, anayesakwa pia na Manchester City na Barcelona (Sun),
Bournemouth wanakaribia kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu hiyo kwa kumsajili mshambuliaji kutoka Wolves, Benik Afobe, 22, kwa pauni milioni 10 (Daily Telegraph),
Everton wanataka kuimarisha ngome yao kwa kumsajili beki wa kulia wa Leeds, Sam Bryam, 22 (Liverpool Echo), West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa Juventus, Simone Zaza, 24 (London Evening Standard), Sunderland wameacha kumfuatilia beki kutoka Ivory Coast Lamine Kone, 26, lakini Aston Villa na Norwich bado wanamtaka (Daily Express),
kiungo wa Newcastle, Cheikh Tiote, 29, anawaniwa na Shanghai Greenland Shenua ya China (Newcastle Chronicle), Stoke City wanafikiria kupanda dau kumchukua mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22 (Guardian). Uhamisho uliokamilika nitakujuza. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumamosi njema!!
 
HIYO HABARI YA SUPER MARIO KAMA HUYO KOCHA ATAMREJESHA SUPER MARIO ANFIELD BASI ITAKUA ANAWAZIMU KICHWANI MSIMU ULIOPITA BALOTELI KAFANYA NINI LIVERPOOL ZAIDI YA VITUKO TUU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom