Ni kweli mkuu. Tetemeko lilikuwa kubwa, maeneo ya SUA. Vitanda vilicheza ila tunashukuru hakuna ripoti za maafa hadi sasaLeo majira ya saa tisa na dakika thelathini na nane usiku (03:38) kumetokea tetemeko la ardhi katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Morogoro,yakiwemo maeneo ya Bigwa,Kolla B,Misongeni Lilidumu kwa sekunde chache sana,ila lilitikisa kweli kweli!mpaka sasa hakuna madhara yaliyoripotiwa kusababishwa na tetemeko hilo.
Tunaomba taarifa kamili kutoka kwa vyonbo husika!
kama kuna mwenye taarifa zaidi, juu ya tetemeko katika maeneo mengine, atujuze
Ni kweli mkuu. Tetemeko lilikuwa kubwa, maeneo ya SUA. Vitanda vilicheza ila tunashukuru hakuna ripoti za maafa hadi sasa
Huku Mazimbu mbona Kama sijahisi kitu.
Mkuu itakuwa ulilala Sana
Nilikuwa macho nacheki Man U vs Inter limetetemesha kweli
Kuna baadhi ya nyumba zimepata madhara ikiwemo nyumba kuezuliwa mapaa,nyingine kubomoka sehemu na nyingine kupata crake!uzuri hakuna taarifa juu ya madhara ya moja kwa moja kama majeruhi kwa wanadamu!