TENZI NA. 24
1. Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu,
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu mwokozi wangu.
Amani moyoni mwangu,
kwa Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe,
Kwa sababu yeye,
Yu nami moyoni mwangu.
2. Sina haja tena, ya kutanga-tanga,
Ndiye kiongozi wangu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu, Mwanawe Mungu.
3. Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
kwa kuwa ninaye Yesu.
Vv