Tengeneza bisi/ndulusi zako mwenyewe

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,890
Huko mjini mnaita popukoni, ni kazi rahisi sana.

Chambua mahindi yako kutoa visivyohitajika hasa pumba ambazo zikiungua huweka weusi kwenye sufuria. baada ya hapo weka sufuria motoni na weka mahindi kiasi. Hakikisha kila punje inagusa kitako cha sufuria, zifunikie ili kuepuka zisitoke nje wakati wa kupasuka na pia uwe unachezesha sufuria horizontally.

Baada ya dakika nne mpiko wako unakuwa tayari na unaweza pika mingine.

Unaweza ukawa unabugia ndulusi zako huku ukiwa jf au unacheki movie. bei ya mahindi ni ndogo sana, kilo ni 1500 na zinatoka popukoni nyingi mno. mi nikikaa bila mahindi ya ndulusi nahisi kama sina sukari au majani ya chai.

toka nimeanza ubuguaji wa ndulusi constipation naisikia mitandaoni tu.
 
si ndo bisi au??
ndiyo hizo hizo mkuu. kitu kizuri kingine ukijiandalia unakuwa unakula za motomoto na siyo viporo vya madukani. wakati wa kupika ni vizuri ukiwa na sufuria za mshikio mrefu au ukaibana na banio la ugali
 
ndiyo hizo hizo mkuu. kitu kizuri kingine ukijiandalia unakuwa unakula za motomoto na siyo viporo vya madukani. wakati wa kupika ni vizuri ukiwa na sufuria za mshikio mrefu au ukaibana na banio la ugali

kwa nini ubane...sina banio la ugali ila nina sufuria za mishiko miwili
 
huko mjini mnaita popukoni. ni kazi rahisi sana. chambua mahindi yako kutoa visivyohitajika hasa pumba ambazo zikiungua huweka weusi kwenye sufuria. baada ya hapo weka sufuria motoni na weka mahindi kiasi. hakikisha kila punje inagusa kitako cha sufuria. zifunikie ili kuepuka zisitoke nje wakati wa kupasuka na pia uwe unachezesha sufuria horizontally. baada ya dakika nne mpiko wako unakuwa tayari na unaweza pika mingine.

unaweza ukawa unabugia ndulusi zako huku ukiwa jf au unacheki movie. bei ya mahindi ni ndogo sana, kilo ni 1500 na zinatoka popukoni nyingi mno. mi nikikaa bila mahindi ya ndulusi nahisi kama sina sukari au majani ya chai.

toka nimeanza ubuguaji wa ndulusi constipation naisikia mitandaoni tu.

Thanks, Vipi naweza tumia "ndulusi" kwa chai?
 
Thanks, Vipi naweza tumia "ndulusi" kwa chai?
mi nimenunua cocoa na kahawa na ninampango wa kula na ndulusi. kwa hiyo nafikiri inawezekana. nchi kama us wanatumia sana corn kwa breakfast.
 
Back
Top Bottom