Nakuunga mkonbo Mkuu,TFF ni waoga sana na haa hawatki kuona watu wenye misimamo wakitua ndani ya TFF,ndio maana unaona hata hivi sasa wanavyofanya kwenye chaguzi za mikoa na vyama vingine shiriki,wanafuta wanavyotaka ama kuwaondoa wale watu ambao wao wanaamini kwamba ni watu wenye misimamo ya ukweli na wa ni ya dhati ktika kuleta mapinduzi ya soka.
Nikupe mifano michache tu hapa,wamebadili Katiba ya TFF na hasa kwenye kipengele cha elimu na hapa sio kwamba nataka kuwatetea wale watu wanaowaita kwamba hawana elimu,hapana!!!!!!,lakini ni uoga tu wa kuwaogopa wakina Abdalah Bulembo na wenzake wengi tu ambao ni watu wanaofahamika kwamba wana hoja na hasa linapofika kitu kinachoitwa maslahi ya wachezaji ama vyama vya michezo vya mikoa!!!!!
Kibaya zaidi hawahawa TFF wamefikia hatua ya kuingilia hadi chaguzi za mikoa na kuwaondoa watu wenye misimamo mikali na ambao wanaona kwamba kwa namna moja ama nyingine wanaweza kuwasababishia kasheshe huko ndani ya TFF na hawa jamaa ni hatari kwelikweli kwa sababu mkoa ambao wanaona kwamba kuna vichwa vingi vimeingia vya hatari na si kambi yao itakayohakikisha mtu wao atakayegombea anashinda wako tayari kuahirisha uchaguzi hata siku ya uchaguzi,mfano tabora,Rukwa na kwingineko!!
Unajua kila kitu na wakati wake,safari hii watu wenye uelewa na msuala ya mpira na wenye uwezo wa kuhoji maswali walijitokeza kwa wingi sana kuwania nafasi za uongozi ndani ya vyama vya mpira wa miguu huku wengi wakiwa wamelenga kwenda kufanya mabadiliko makubwa wakati wa uchaguzi wa viongozi wa TFF ikiwa ni sanjri na kuhoji maswali tata yaliyoko TFF.
Jamaa walipogundua hilo wameamua kuharibu chaguzi nyingi za mikoa mfano tu jana wamezuia kwa mara ya pili uchaguzi wa viongozi wa waamuzi FRAT kwa sababu tu watu wao hawana uhakika wa kushinda na ndivyo ilivyoonyesha baada ya wajumbe wa FRAT kukaidi agizo la kuzuiwa kufanya uchaguzi na kufanya uchaguzi wao.
leo hii wanakuja na CAF imesema masuala ya marekebisho ya katiba,kanini uchaguzi usifanyike halafu hayao masuala ya marekebisho ya uchaguzi yatafanywa na uongozi utakaochaguliwa???!!!!,hivi hapa kuna logioc ya kusababisha uchaguzi uahirishwe hadi mwezi wa pili mwakani,au ndio wanataka FIFA iingize zile shilingi Milioni 800 za kila mwaka kwa ajili ya maendeleo ya soka nchini wazitafune kwa mara ya mwisho,au zitumike kuwahonga wajumbe????!!!!
Jamani watu wamekuwa wakilalamika sana juu ya masuala ya UFISADI!!!!!!!!!UFISADI hauko CCM tu hata ndani ya TFF hebu fikiria FIFA wanaleta kila mwaka shilingi milioni 800 kwa ajili ya maendeleo ya soka halafu leo hii bingwa anapatiwa shilingi milioni 40!!!!!!!!!!!!!!!Aibu iliyoje ndugu zangu???????!!.
VODACOM wametoa zaidi ya shilingi Bilioni 1.4 kila mwaka halfu bingwa anapatiwa shilingi milioni 40,jamani eeeeeeeeeee inauma sana!!!!!!,pamoja na kwamba sina masters ya Accountat lakini kuna hesabu ya harakaharaka ukiifanya hapa unagundua kamba ni kwa nini wakina Tenga wanadaiwa kumiliki Magorofa Dar????!!!!!!!,wanafanya kazi ya kugawana tu fedha za wachezaji,haiwezekani zaidi ya shilingi Bilioni 2 wanapata kila mwaka kutoka FIFA NA VODACOM Tanzania washindwe kuinua mpira wa Tanzania,ni wazi kwamba haingii akilini,lakini waswahili walinena kwamba siku za mwizi ni 40,tayari Arobaini yao imefika kikubwa hapa ni kuapa nguvu tu hawa wapambanaji waliojipambanua kupambana nao.
kwa leo ngoja niishie hapa lakini naamini nitapata muda mwingine wa kutiririka zaidi kwa sababu nina data zao za kutosha,na ukitaka kuamini hili ninalolisema,mchunguzeni Mwakalebela alivyo tajiri au hata Tenga mwenyewe aliingia na shati moja siku ile pale kwenye ukumbi wa Golden Tulip leo anamiliki zaidi ya magorofa matatu Dar!!!!!!!!!!!!!!!