Tembo aliye chumbani hazungumziwi, je tutafika?

salaama

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
251
325
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano amepokea taarifa ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma. Kwenye taarifa hiyo imethihirika watumishi elfu tisa 9000 walikuwa na vyeti vya kufoji....

Kwa jamii ya watu makini,ingetegemewa uwepo mjadala mzito uliosheheni masuala ya msingi kama vile:
1) Tumefikiaje hatua ya kuwa na watu 1,2,3,4 mpaka 9000 wameingia kwenye ajira ya serikali kwa vyeti vya kufoji...

2) Waliohusika kuajiri watu hao watachukuliwa hatua gani

3) Kwanini waliofoji vyeti wasichukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine

4) Kuna tatizo gani la msingi ndani ya jamii yetu hadi kufikia kuwa na watu wasiothamini umuhimu wa elimu na kutafuta njia za mkato wakati wenzao waliosoma ipasavyo wanakosa fursa za ajira

5)Nani awajibike kisiasa kwa upungufu huu mkubwa uliotokea

6) Tunaipongeza serikali kwa kuonyesha njia kufanya uhakiki na kuweka hadharani matokeo...je kwenye sekta binafsi wapo wangapi wa aina hii (waliopata ajira kwa kufoji vyetu...

Maswali ya kujiuliza kama taifa kwa tukio hili zito linaloweza kuitwa JANGA la kitaifa ni mengi. Lakini kwa bahati mbaya magazeti, mijadala ya social media imepoteza mwelekeo, badala ya kujielekeza kwenye maswali ya msingi juu ya watu 9000 waliofoji ambao kwa uzito ndio ninawaita TEMBO NDANI YA CHUMBA, mijadala imeelekezwa kusiko na tija kwamba kwanini wanasiasa hawajahakikiwa, wakuu wa mikoa na wilaya sio wanasiasa etc. Ndio hayo maswali yana merit,lakini kwa uzito wa watu 9000 kubainika kufoji vyeti, pengine mjadala wa hayo ungekuja baada ya wiki moja ya mjadala wa ajenda kubwa ya watu 9000...imekuwaje...tunaelekea wapi....kinachoendelea kupitia mijadala mbalimbali hivi sasa ni sawa sawa na kupata taarifa ya Msiba wa mtu aliyepata ajali ya akiwa kwenye pikipiki na kufariki kwa kukosa helmeti kichwani.........badala ya mjadala kujielekeza kwenye tatizo la msingi la ajali za barabarani na kutofuata sheria kunakofanywa na waendesha pikipiki, mjadala unajielekeza kwenye uchakavu wa uniform za trafiki....ndio inawezekana kuwa ni kweli trafiki kutovaa uniform nadhifu kunaweza kumkatisha tamaa ya kazi, lakini hakuzuiii kuongelea tatizo la msingi la waendesha bodaboda kutovaa helmet kulikosababisha vifo vingi...

Tafsiri ya watu 9000 kufoji vyeti na kupata ajira inatafsiri kwamba sisi kama taifa tumeshaona ni kawaida kuchukua njia za mkato kufanikisha ajenda uliyonayo,hata kama ni kwa kuvunja sheria. Kweli Rais Magufuli ana kazi kubwa sana ya kunyoosha mambo, badala ya kubeza hatua zake ambazo manufaa yake ni long-term anapaswa kuungwa mkono na kusaidiwa.
 
Hii nchi maadili yalisha potea,vyeti feki ni moja tu,sheria ya hii nchi ina saidia utapeli,mfano cheki feki hivi sasa ni madai na siyo kosa la jinai,imefanya biashara kuwa ngumu hii nchi kwa watu waadilifu,mtu akikutapeli unaambiwa ni madai nenda wilaya anayoishi ukafungue kesi,inamaana kama anaishi kigoma wewe uko dar wewe ndiyo usafiri kudai mali yako.
 
Kwanza nakupongeza kwa hoja nzuri lakini nikukumbushe lini Rais wetu au chama cha ccm kiliwahi kupokea ushauri?Iko wapi katiba ya Mhesh. Warioba?Kuna ushauri mzuri kama ule wa wananchi? Ccm waliacha ya wananchi wakaweka ya kwao mbele ya maprof n.a. madoctor wengine walizikana thesis zao wenyewe Dr Mwakyembe Prof Hirji nk mpaka tutakapokiri tz kwanza n.a. siyo chama hayo/hizo hoja zako nzuri ndipo tutakapo zifanyia kazi na inawezekana kama JPM akitaka hivyo na akubali kudili na akina bashite ndipo kazi/ni yake utakapopata hadhi.
 
Hii nchi maadili yalisha potea,vyeti feki ni moja tu,sheria ya hii nchi ina saidia utapeli,mfano cheki feki hivi sasa ni madai na siyo kosa la jinai,imefanya biashara kuwa ngumu hii nchi kwa watu waadilifu,mtu akikutapeli unaambiwa ni madai nenda wilaya anayoishi ukafungue kesi,inamaana kama anaishi kigoma wewe uko dar wewe ndiyo usafiri kudai mali yako.
Kwahiyo maadili yakipotea, Serikali isishughulikie kunyoosha mambo?
 
Si
Kwahiyo maadili yakipotea, Serikali isishughulikie kunyoosha mambo?
Siyo serikali ya CCM,Tuko hapa baada ya miaka 50 ni ulaghai,wizi,fitina,wizi,Zaidi ya 50% ya nyumba za serikali ni za wizi (kutaifisha) unategemea vizazi hivi vitakuwaje?sheria ya dhulma,nyumba za dhulma halafu vizazi waadilifu watatoka wapi?
 
Si

Siyo serikali ya CCM,Tuko hapa baada ya miaka 50 ni ulaghai,wizi,fitina,wizi,Zaidi ya 50% ya nyumba za serikali ni za wizi (kutaifisha) unategemea vizazi hivi vitakuwaje?sheria ya dhulma,nyumba za dhulma halafu vizazi waadilifu watatoka wapi?
Ndio kusema hatua anazochukua Rais hauzioni? Au kwakuwa anatoka CCM unafumba macho kuziona na kukubali kwamba anasafisha nchi. Kazi ya kusafisha sio lele mama, sio rahisi, ina machungu mengi. Hatuwezi kutaka mabadiliko,hapo hapo yanapotokea tunalalamika
 
Back
Top Bottom