MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,997
Nianze kwa kusema, Tundu Lissu ni mwanasiasa mjanja sana na kama ukitaka kufanya anachokifanya unaweza kujikuta unaangamia kisiasa au kimapato.
Inaonekana pia vyombo vikuu vya habari nchini hasa televions vimeishafahamu ujanja wa Tundu Lissu na madhara ya kufanya au kutangaza kile ambacho Tundu Lissu anakifanya au kukisema kuhusu utawala wa awamu ya tano. Hakuna television inayopenda kuwa accessory to a crime au kutukana wakunga na uzazi ungalipo!
Hii imedhihirisha jana baada ya Tundu Lissu kuongea maneno ambayo kisheria hana kosa hata kama ukimpeleka mahakamani lakini kisiasa yalionekana yanamlenga Rais wa Tanzania katika mlengo wa kumbomoa kisiasa hata hivyo vituo vyote vya Television vikampuuza. Lengo la maneno yake ninadhani ni kuwapandisha mzuka wanazi wa kisiasa wale ambao hawafahamu vizuri sheria.
Fani yake ya sheria inamuwezesha Lissu kuchagua maneno ya kusema kwa uangalifu bila kuvunja sheria wakati huo huo yakimjenga kisiasa. Ieleweke kuwa mwanasheria anayeogopa kuvunja sheria anazodai ni kandamizi, huyo siyo mpiganaji halisi bali ni professional coward.
Tundu Lissu is good at searing political rhetoric and bloated back-slapping!
Katika maongezi yake yote baada ya kutoka mahakamani, hakutamka neno ‘’Rais wa Tanzania’’ au ‘’jina la Rais wa Tanzania’’ kwa maksudi bali alijikita kwenye neno ‘’dikteta uchwara’’ huku akionyesha kama vile hamfahamu vizuri dikteta uchwara baada ya kusisitiza akisema, ‘’huyu dikteta uchwara akabiliwe kokote aliko’’. Kwa maelezo haya mahakama huru haiwezi kumkuta na hatia yoyote.
Hata ukimkamata na kumpeleka mahakamani ataenda kukuuliza wewe ulifahamu vipi kama nilimsema Rais wa Tanzania wakati sikutaja neno 'Rais wa Tanzani' au Jina la Rais wa Tanzania? Unafahamu vipi kama Rais ndiye dikteta uchwara? Vigezo gani umetumia kufahamu kama Rais ni dikteta uchwara? Umefahamu vipi kama maagizo yanatolewa na Rais wa Tanzania?
Ninakumbuka baada ya Uchaguzi Mkuu 2010, kuna baadhi ya wanasiasa walianza kuiga style yake ya kisiasa lakini baadaye wakagundua itawaangamiza kisiasa na wameamua kuachana nao. Mmojawapo ni Godbless Lema ambaye kwa sasa amekuwa kama born again politician.
Godbless Lema is borrowing a leaf from Immanuel Kant once says experience without theory is blind, but theory without experience is mere intellectual play!