Don jully
Member
- Jun 12, 2013
- 50
- 66
Kumekuwa na matukio mengi yanayoendelea hivi karibuni na watu kwa kujua ama kutokujua wamekuwa wakitekeleza roho za kishirikina. Mathalani kumekuwa na wimbi la watu kurekodi matukio ya udhalilisha, aibu, uovu na hata mambo ya hovyo.
Siku hizi ni fashion kurekodi matukio maofisini, majumbani na hata kwenye hadhara na kuweka kwenye mitandao bila kujali matokeo yake ama kwa kutimiza adhma husika.
Siku hizi kama mtu akiwa na lengo au nia mbaya juu yako anaweza kusubiri ama kukutegea ufanye jambo lolote litakaloweza kutimiza malengo yake na kuweka group la WhatsApp na kusubiri matokeo yake.
Mwisho wa yote group lina watu wengi ambao wengine hawajui agenda ya aliyerekodi ni nini, wanajikuta wanapost kwenye mitandao mingine ya kijamii.
Boom! Watu wanasimamishwa kazi, kuachishwa kazi, kuchunguzwa, kudharauliwa, kukamatwa na mambo mengine mengi. Roho ya kishirikina imefanikiwa.