Hapo ndipo tofauti ya tecno na simu nyingine inapoonekana ie HTC ONE, SAMSUNG S1..... Kitu ulichoelezwa ni sawa lakini kuna application za kuhamisha sio zote zinakubali kwenda kwenye SD, na nyingine zinakuwa automatic installed kwenye internal memory. Kwa hiyo kama ni mtu unaependa sana kuinstalled applications nyingi kwenye cmu tecno sio mahali pake waache watu wanaoishia kwenye WhatsApp, viber, telegram, Nimbuzz, wechat etc lakini kama unataka kuweka vitu vingi sana tafuta cmu yenye internal kubwa. Wajanja walishaona hilo tatizo ndio maana utakuta simu kama htc one ina internal ya 32GB, samsung s4 16GB, sasa kuna mtu atakwambia mimi cmu ya internal memory ya 2GB inatosha akishazoea tu anaona haimfai tena. Utakuta kuna msg Update available ukiclick kuinstall utaambiwa memory full aisee unaichukiaje cmu. Hapo bado issue ya speed ya processor lazima urudi kwenye cmu za maana. Wewe inaonekana ni mtu wa kupenda application nyingi nakushauli uza hiyo cmu waachie wageni wa technologia wewe umeshakuwa mzoefu chukua kitu cha maana.