Kama mzee wa mia bab
figganigga alivosema hapo juu, lazima kwanza uwe umejiunga na account ya gmail kuweza kudownload hizo applications ulizozitaja katika Google Play.
Pia hakikisha simu yako ina internet connection. Sasa swali je, umeshajua kuconnect?
Kama tayari, nenda Google Play au unaweza kuta imeandikwa Market, kisha ingia. Utaona wamekuambia Login with Gmail. Kama account ya Gmail unayo, ingiza hapo, email and password. But kama huna, chini yake utaona Create Account, fungua hapo kisha jaza jza hizo form upate account yako ya Gmail. Dakika 10 tu umemaliza.
Ikifunguka (Hiyo Google Play Store), upande wa kulia juu kuna alama ya search (kama lensi ya kuchungulia), hapo ukiclick utaandika application yoyote utakayohitaji kama Fb, Whatsapp, Viber, JamiiForum etc.
Ikija download then itajifanya vingine automatic.
Kama kuna internet na umesema inasema TimeOut. Na wasiwasi na speed ya internet mahala ulipo. Jaribu kutafuta sehemu yenye 3G/HSDPA.
Karibu Android kaka.