Technical advice ya namna gani Kwa huyu kijana ili ajishughilishe?

UMASIKINI BWANA

JF-Expert Member
Oct 17, 2013
942
566
Hi the greatest thinkers kutoka pande zote East Africa na kwingineko duniani.

Kuna ndugu yangu Fulani ni mbishi yupo kijijini alifeli kidato cha NNE.Ana miaka minne mtaani kurudia hataki.

Nikamshauri aende veta ndugu tukajichanga kapiga hela na mademu kalizimia kwenye gia.Nikamshauri jifunze welding udereva au hata utingo kaziba masikio.

Vijana wenzie wanachakalika wanapata riziki yeye misele kitaa kiburi mtindo mmoja anasubiri vya kupewa.

Kumuacha nashindwa inafikia ananichukia eti nampigia kelele lkn Kwa faida yake hivi sasa kajaza mimba mtoto wa watu kitaani

Sasa Jf ni sehemu ya watu wenye akili sana je ni technical advice gani ama ikiwezekana intelligence itumike ama brain washing pia itumike ili asije amka kumekucha.Karibuni sana waungwana.
 
Back
Top Bottom