Team Lowassa itakwepwaje? Watatenda kwa haki?

Team Lowassa itakwepwaje? Watatenda kwa haki?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Ndani ya CCM, kuna Wabunge wanaomuunga mkono aliyekuwa mgombea wa Urais wa CHADEMA/UKAWA, Ndugu Edward Lowassa. Wapo waliojipambanua mwanzoni na mwishoni 'ku-act' kama wamemuacha mkono na kujiunga na aliyekuwa mgombea wa CCM, Rais Magufuli. Hapa waweza kutajwa akina Peter Serukamba, Hussein Bashe na Kangi Lugola.

Pia, wapo wale Wabunge ambao hawakuwahi kujipambanua hadharani kuwa wanamuunga mkono Lowassa. Lakini, kuanzia wakati ule hadi sasa, wao ni wafuasi wa kutupa wa Lowassa. Baada ya kupendekezwa na kuidhinishwa kwa Waziri Mkuu, Rais akishauriana na Waziri Mkuu atateua Baraza la Mawaziri.

Wale team Lowassa watakwepwaje? Wakiingia Serikalini kama Mawaziri au Manaibu Mawaziri watatenda bila kikwazo? Najiuliza tu

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Hao hao Team Lowassa wastaafu kama Msukuma,Bashe na Lugora ndio walikuwa wanamtukana EL ubavuni mwa JPM!
 
Shiiiiiiiiiiiiiiiii! Shiiiiiiiiiiiiiiiiiii! kimya kimya! Tulia usigeuke mbele wala nyuma!

Tuache! Endelea kufuatilia mchezo! Hadi sasa Magu anatafuta mpira kwa tochi!

Hii ni champions league! Magu hawezi ligi kubwa hizi!
 
Imarisheni ukawa ya ccm hamuyawezi tena,atakaeonekana ni msaliti atakatwa mara moja
 
Hao Team Lowassa ndani ya CCM ni wa kuwakwepa kama ukoma endapo Magufuli anataka ufanisi katika serikali yake.

Naamini wapo watu makini na waadilifu ambao si team Lowassa. Ikibidi ateue wabunge na kuwaingiza baraza la mawaziri. Muhimu iwe kuwatumikia watanzania.
 
Tumeshawakata tulieni acheni kujibaraguza!!

CCM ni taasisi sio mtu...
 
Hapo inabidi muwe makini, vinginevyo MZEE TUPATUPA na CCM yako mtapata shida!
 
TeamLowassa ilishashuka daraja!!!
Hakuna kitu kinachoitwa "wanaomuunga mkono Lowassa" ndani ya CCM kwa sasa!!!
Na wewe una jifanya mwana CCM wa hapo Dodoma makao makuu ndio unataka ku create makundi ambayo kwa sasa hayana nafasi tena!!!
Mimi mwenyewe nilimuunga mkono huyo Lowasa wakati ule Dodoma kwenye vikao vya kupitisha mgombea Uraisi!
Lakini nakuambia ukweli, timu Lowasa imebaki ni nadharia tu kwa sasa lakini kiuhalisia haipo tenaa!!!!
Kama unakumbuka Lowasa alipo kuwa Mbulu kwenye mkutano wa kampeni za Uraisi kupitia CDM alisema rafiki wake wa kweli ni yule aliyemfuata huko UKAWA na kwamba yeyote aliyebaki CCM siyo rafiki yake tena!!!!!!!!!!!
Acha siasa za kizandiki!!!!!!
 
Hao Team Lowassa ndani ya CCM ni wa kuwakwepa kama ukoma endapo Magufuli anataka ufanisi katika serikali yake.

Naamini wapo watu makini na waadilifu ambao si team Lowassa. Ikibidi ateue wabunge na kuwaingiza baraza la mawaziri. Muhimu iwe kuwatukia watanzania.

Kwa kura za uspika za jana nadhani ukiwa nje ya ccm si mwenzao tena linapokuja suala la maslahi ya chama. Ole Medee asingepata kura hizo kama kweli Lowasa bado ana ushawishi kwa wabunge wa ccm.
 
Kwa kura za uspika za jana nadhani ukiwa nje ya ccm si mwenzao tena linapokuja suala la maslahi ya chama. Ole Medee asingepata kura hizo kama kweli Lowasa bado ana ushawishi kwa wabunge wa ccm.

Waambie ukweli. Urafiki kwenye siasa hakuna. Chama ni zaidi ya mtu mmoja mmoja
 
Hii ni nini sasa??!!
Ina maana waliompigia kura Lowassa wanatakiwa watoke serikalini??!! Au kazi ni uwaziri na unaibu tu??!!
Vipi makatibu wakuu??!
Wakurugenzi??!!
Mabalozi??!!

Acheni serikali iundwe wananchi watumikiwe hii nchi sio ya Lowassa wala Magufuli sijui kwa nini mnataka hii dichotomy iingie kila mahali??!!
Ukienda hospitali unauliza nesi na dokta ni timu gani??!!
Ukipanda chombo cha usafiri unauliza owner na operator ni timu gani???!!

Msiendekeze kugawa Taifa bila sababu za msingi
 
Kikwete mbona hakufukuza team Mwandosya wala team Salim?

Magufuli atajiongezea maadui unnecessary.....
 
Tunayo hiyo list na itaishia tu ubunge na uwenyeviti wa kamati za bunge.
 
Ndani ya CCM, kuna Wabunge wanaomuunga mkono aliyekuwa mgombea wa Urais wa CHADEMA/UKAWA, Ndugu Edward Lowassa. Wapo waliojipambanua mwanzoni na mwishoni 'ku-act' kama wamemuacha mkono na kujiunga na aliyekuwa mgombea wa CCM, Rais Magufuli. Hapa waweza kutajwa akina Peter Serukamba, Hussein Bashe na Kangi Lugola.

Pia, wapo wale Wabunge ambao hawakuwahi kujipambanua hadharani kuwa wanamuunga mkono Lowassa. Lakini, kuanzia wakati ule hadi sasa, wao ni wafuasi wa kutupa wa Lowassa. Baada ya kupendekezwa na kuidhinishwa kwa Waziri Mkuu, Rais akishauriana na Waziri Mkuu atateua Baraza la Mawaziri.

Wale team Lowassa watakwepwaje? Wakiingia Serikalini kama Mawaziri au Manaibu Mawaziri watatenda bila kikwazo? Najiuliza tu

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Kwa mawazo yako we unafikiri hawajulikani?
Kwanza we mmoja wapo.
 
Kwa kura za uspika za jana nadhani ukiwa nje ya ccm si mwenzao tena linapokuja suala la maslahi ya chama. Ole Medee asingepata kura hizo kama kweli Lowasa bado ana ushawishi kwa wabunge wa ccm.
Umemaliza. Ujumbe tosha kwa wapumbavu wote.
 
Sasa ng'ombe mzima wote kalika, Mh Rais ashindwe na mtu mmoja mmoja wakati ameshakishinda chama kikubwa? tuweni wakweli Watanzania.
 
Tumeshawakata tulieni acheni kujibaraguza!!

CCM ni taasisi sio mtu...

Unachekesha sana! yaelekea hujui hata kinachoongelewa. Mfano, Sophia Simba mmemkata Ubunge au unijichetua tu hapa???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom