Team Lowassa, a lemon should make a fine lemonade

Team Lowassa, a lemon should make a fine lemonade

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2010
Posts
1,948
Reaction score
1,238
Ni wazi kuwa sasa kutokana na ule mtikisiko dhahiri ulioonekana jijini Dar es Salaam wakati mgombea urais wa Ukawa ndugu Edward Lowassa akienda NEC kuchukua fomu za kuomba kugombea urais, serikali iliyo madarakani kupitia kwa jeshi la polisi imeanza kuweweseka na kuanza kufanya mbinu za kuhakikisha wananchi hawaoni jinsi ambavyo mgombea huyu anakubalika na hivyo kupunguza hamasa kwa wananchi wengine.

CCM daima wamekuwa ni watu wa kutumia mbinu chafu kwenye kuhakikisha wanakuwa na advantage kwenye kura hata kama ni kwa kupitia njia isiyo sahihi. Ninakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ilivyopiga marufuku midahalo ya wagombea wake wa Ubunge pamoja na Urais kupitia TBC kwa kujua dhahiri kwamba wagombea wengi wa CCM wangeaibika mbele ya wananchi kutokana na kuwa na mengi ya kujibu kulikosababishwa na utendaji mbovu uliokwisha shuhudiwa kutoka kwao miaka mitano iliyotangulia. Waliishia kumfukuza kazi mkurugenzi wa TBC kwa kuruhusu midahalo hii jambo ambalo ni la ajabu na kibabe kuliko inavyoweza kuelezeka ikizingatiwa kuwa duniani kote midahalo ya televisheni ndio njia kubwa kuliko zote za wagombea kutangaza sera zao kwa wapiga kura.

Inashangaza kwamba miaka 55 baada ya uhuru wetu kiongozi wa upinzani na waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri yetu anazuiwa kwenda kwenye msiba ati kwa sababu amefuatana na watu wengi..kweli kabisa?!? Wakati huo huo jeshi la polisi likitangaza kupigwa marufuku maandamano ya wananchi kumsindikiza mgombea kuchukua au kurudisha fomu za urais au kuomba ridhaa ya kugombea kwa wananchi. Ni wazi haya yote yanafanyika ili kuwaficha wananchi ukweli kwamba mgombea wa CCM hakubaliki na watu wengi ili kurahisisha mipango ya kuiba kura ifikapo Octoba.

Mimi nadhani wakati umefika sasa kwa viongozi wa Ukawa kukuna vichwa na kuhakikisha wanatumia magumu haya kujiongezea umaarufu zaidi. Nitatoa mfano. Wakati EL aliposimamishwa na kuzuiwa kwenda kwenye msiba jana mchana, ilikuwa ni nafasi nzuri ya kusimama bila kuchelewa na kutoa hotuba yenye msisimko ya kuwakumbusha wananchi jinsi kitendo hiki kilicho cha ajabu na fedheha kubwa kinavyosimamiwa na uongozi wa juu wa CCM ili kumlinda kiongozi wasiyemtaka. Viongozi wa Ukawa inapasa sasa kutembea na vipasa sauti popote waendapo ili elimu hii ya uraia iweze kutolewa papo kwa papo kwa wananchi na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni kuwezesha wananchi wengine waone.

Wakati wa urudishaji fomu za NEC ninashauri kwanza itizamwe njia itakayotumiwa na mgombea wa CCM. Ikiwa hakutakuwa na maandamano kabisa basi Ukawa wanaweza kuwaandaa wananchi zaidi ya wale waliojitokeza wakati wa kuchukua fomu kuhakikisha wanasimama pembeni ya barabara karibu na ofisi za NEC na njia zote kuu atakazopita mgombea wa Ukawa ili kuhakikisha watu wanapata nafasi ya kuonesha upendo wao kwa mhe. Lowassa bila kusababisha maandamano.

Vyoyote iwavyo, kwa mbinu yoyote chafu waitumiayo CCM kupitia vyombo vya sheria na usalama kuzuia mafuriko, kuna haja ya kuitumia kwa uangamivu wao zaidi. Siasa mufilisi hazina nafasi tena kwenye nchi yetu.

Ukipewa malimao kamua juice nzuri sana ya malimao umkaribishe aliyekupa.

Victory has arrived. We are the change we had been waiting for.
 
Barua ya Jeshi la Polisi ambayo imetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Z.Msangi ikikataza maandamano na kukubali kufanyika kwa mkutano tu.

Tangazo kwa umma
Mnamo tarehe 10/08/2015 ofisi ya mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya ilipokea barua toka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya Ruanda nzovwe. Lengo la mkutano huo ni mgombea wa Rais kuomba wadhamini Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilikutana na uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo akiwemo mbunge wa mbeya mjini na baadhi ya madiwani katika eneo la usalama wa chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano. Hii inatokana na; Sababu za kiusalama Kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja.

Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki.hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Haya nyingine hii - completely preferential politics - Mbeya kuna msongamano gani wa magari hata maandamano haya yaharibu shughuli za kawaida za kila siku? Huyu ni yule Ahmed Msangi aliyepanda cheo baada ya kuhusihwa na utesaji?
 
CCM ipo ICU hawana jinsi wanahaha tu...wenye akili wote ndani ya CCM wametulia kimya wamemuachia Kikwete coz anawaona wajinga.
 
Dawa ni kujipanga barabarani watu waoneshe mapenz kwa rais wetu mtarajiwa....hawawezi kuzuia mafuriko kwa mkono
 
Ndio maana Kagame anapata justification ya kumrushia vijembe rais wetu kuwa anahubiria demokrasia lakini anaikana kwa vitendo
 
Back
Top Bottom