Hii ni nchi ya vituko na maajabu.
Yaani Elimu imekuwa ndio sehemu ya kufanyia majaribio.
Miezi mitatu iliyopita GPA ya kuingia chuo kikuu ilikuwa 2.5, ghafla ikabadilishwa na kuwa 3.5 na leo ni 3.
Serikali ya mwendokasi! Wanasiasa wanakimbilia kwenye media kutoa matamko yanayokinzana na utaalamu, matokeo yake ndio hayo watu wanapindua matamko baada ya muda mfupi!
trump gets his degree from the university of Pennsylvania and hillary clinton gets her degree from yale... wote ivy league......ila hawa wa kwetu wazee wa matamko wamepata vyuo vya mwendo kasi. tuwavumilie tu
Elimu ya tanzania haina ubora kila mwaka inachezewa kisiasa mara BIG RESULT NOW , mara wakaanzisha DIVISION 4 inafika mpaka 40, mara GPA inajitune yenyewe kama vile kama redio za mchina teh hii nchi ingie tu kwenye maajabu ya dunia
Serikali ya mwendo kasi, mwezi July walitoa waraka kuwa kidato cha pili hakutakuwa na mchujo, mwezi huu September wamekuja na waraka tena eti mitihani uko pale pale na mchujo uko pale pale..... Kwenye GPA nako, mkurupuko at work