Mligo Augustino
Senior Member
- Nov 29, 2017
- 126
- 278
Kwanza kabisa tunawapongeza TCU kwa kazi nzuri ya kuboresha elimu ya juu nchini. Hata hivyo TCU inatakiwa kubadilika ktk sera zake kulingana na mahitaji halisi ya nchi na jamii ya wakati husika:
1.Syllabus za elimu ya juu bado zipo kizamani. Taaluma inayofundishwa vyuoni haimuandai kijana kujiajiri na kupambana na mahitaji ya nchi na dunia ya sasa. Elimu ya juu imekuwa ni ya madesa tu na kukariri. Na kipimo cha mtu kuwa msomi ni marks tu. Hili ni tatizo kubwa sana kwa usitawi wa nchi. Ndiyo maana tuna wasomi wengi wa vyeti, lakini hawawezi kutatua matatizo.
2.GPA ya 3.5 undergraduate kuwa ndo kigezo msingi cha msomi kufundisha chuo kikuu. Kigezo hiki kimechangia vijana wengi hasa waliohitimu vyuo vikuu vya serikali ambao wanauwezo mkubwa ila GPA iko chini, kushindwa kujiendeleza zaidi kwa hatua ya PhD.Matokeo yake baadhi ya kada kuna upungufu mkubwa sana wa wahadhiri.Ni wazi wahitimu wa vyuo vikuu vya binafsi hupata GPA za juu.
NACTE GPA ya kumfanya mtu afundishe vyuoni ni 3.0.Je kwa nini TCU nao ikiwa GPA ya 3.0 ili kutoa fursa kwa vijana wengi kupata hamasa ya kufanya masters degree na hatimaye PhD? Kwa sababu vyuo vya NACTE vingine vinatoa hadi PhD.Je msingi wa ubaguzi/utofauti huu ni nini?
Kuanzia mwakani haya mafuriko ya elimu bure yatahamia vyuo vikuu kwasababu kundi la kwanza la form 4 wanamaliza mwaka huu(hongera kwa serikali). Je kwa sera hii ya TCU ya kung'ng'ania GPA ya 3.5 tutafika? Wahadhiri watatoka wapi?
Pendekezo:
1.Syllabus za vyuo vikuu ziangaliwe upya na haraka ili ziendane na mahitaji ya wakati.
2.NACTE na TCU wote wawe na GPA ya msingi moja, yaani 3.0.
3.Vyuo vipewe mamlaka zaidi ya kuamua nani anafaa kuwa mwalimu wa chuo kikuu, kulingana na uwezo wake aliouonyesha wakati wa interview. Na interview iwe progressive mpaka madarasa mbele ya wanafunzi.Wahadhiri wasipimwe kwa GPA tu, bali kwa performance. Tunashudia watu wana GPA kubwa lakini akiingia darasani anahema tu na kutoka jasho. Tunajiuliza hii GPA kubwa alipateje? Wanafunzi wanahitaji mwalimu mwenye uwezo mzuri wa kufundisha, siyo mwenye GPA 5.