TCU: Darasa la saba sasa kujiunga na chuo kikuu moja kwa moja

harufu Uliyonusani Sahihi kwani Kuna Water wanataka kupachikwa Ubunge 2015 nakisha uwaziri lakini hawana Uwezo na katiba ijayo Itawabana

Ina maana sheria mama imebadilika....?! Zamani mbona ilikuwa mgombea ubunge sharti ajue kusoma a e i o u.
 
duh, hii ni fursa kwa vipanga waliokosa nafasi kuendelea na elimu ya juu. kwagu nina house girl kipanga vibaya nataka nimwandikishe ajaribu hiyo paper!!
 
Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:

“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”

Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.

“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Sishangai tumechelewa tu ipo mifumo mingi inayoweza kwafaikisha wanataaluma mbalimbali katika ngazi za juu hasa ukizingatia nchi hii ni duni katika kila nyanja pamoja na utajiri wote uliopo.

Mfano nchi ya korea ya kusini ilifanikiwa kwa kuanza kuwapa elimu hata wale ambao hawakusoma kabisa ili waweze kutumika katika viwanda mbalimbali nchini mwao, wao waliazimia kuwekeza katika rasilimali watu kwa kuwaendeleza.

nchi za ujerumani,Italy china,Urusi nazo zilifanya vivyo hivyo kwa kuamini kuwa mtu mwenye taaluma fulani na akadumu hapo pamoja na kozi shiriki mbalimbali basi ana uwezo wa kuendelea mbele pasi shaka yoyote.

mfumo tuliorithi toka kwa waingereza ndio umetufifisha akili yetu na kudhani formal education ndio hiyo tu inayoweza kutambuliwa na kukubaliwa katika mifumo yetu.
 
Heeeh!!!!
Huuuu!!!!
Hiii kali sijapata kuona dunia nzima..
Inamaana waandishi wa rekodi za dunia kwenye kitabu cha Guiness hawajaliona hili?..
any way nikpata adress zao ntawapa taarifa..
 
Heeeh!!!!
Huuuu!!!!
Hiii kali sijapata kuona dunia nzima..
Inamaana waandishi wa rekodi za dunia kwenye kitabu cha Guiness hawajaliona hili?..
any way nikpata adress zao ntawapa taarifa..
utachekwa wewe mfumo umeanzia huko huko unakotaka kupeleka huo umbeya USA,UK,france etc kote mfumo huu upo hapa tz si roho mbaya tu ya kutaka kuwanyima watu fursa ndio inapinga
 
Let your role model be a successful person. Kuna engineers na degree zao hawawezi ku-set foundation ya jengo wakati experienced mason anaweza tena kwa usahihi mkubwa kwa nini kama wanaweza kusoma na wakafaulu wasipewe nafasi?

naungana na wewe,kuna vijana wanachukua injinia ya mining,huwa wakija field nawapiga msasa mpaka wananiuliza uinjinia wangu nilisomea wapi,kumbe mie form tatu tu.kwa upande wangu mimi najiandaa kujoin chuo mara moja.asante TCU.
 
Kuna watu wanao uwezo mkubwa sana na walishia la saba tuu. Na kuna mambumbumbu kibao yalitoboa kimazabe na mpaka yakafika chuo kikuu hivyo hivyo, kwahiyo mi nnaiunga sana mkono hii mpango jamani, kuna mitihan kule wasojiweza watadunda tuu. Mbona wapo wanaofaullu semista zao kwa kuonga ngono???
 
safi sana!! kwa mtindo chadema hawana chao! kufikia Sept 2015 wheshimiwa madiwani wetu, wakulima na ma barmade watakuliwa wanakula nondo!! kura kwa ccm 2015.!
 
Hivi TCU fikra hizi wametumwa na MUNGU? maana ni kama njia mpya ya ukombozi, watu wataachana na kurudia mitiani ya form four yaani PC kwani PC ni Mtambo wa kufilisi akili na kujiongeza kipato kwa kupitia NECTA, watu wengi wanang
ang'ania masomo magumu kumbe wanaweza kujikwamua kirahis kwa kusaka vipaji kupitia njia hii.
 
Huyo Dr.Maronga ni kilaza mmoja ambaye TCU wamemtoa kutoka UDSM, alishawahi kunifundisha ni kilaza niaje!!! Hiyo idea sio practicle ila imejaa nadharia nyingi, tukitaka tuendelee kuharibu elimu ya hii nchiiii basi tujaribu huu ujinga!! kwi kwi kwi kwi kwi kwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Maronga bana? Naanza kuwa na mashaka na Doctorate yako!!
 
Labda!!!! na hiyo tutaiitaje cjui mayb elimu MSETO& itakuwa vurugu katika nchi hii, ngoja tusubiri tuone utekelezaji wake
 
Katika mfumo huu wa serikali ya chama cha magamba ama kweli hata uwe profesa au dokta ni lazima elimu yako uiache nje ya system.This is shit kivipi std seven awe chuo kikuu.
 
Bado siamini hiki ninacho kisoma kama ni cha kweli au macho yangu, au sijui ni kweli mleta uzi ame mnukuu huyo jamaa au kaamua kuandika ya kwake, yaani STD 7 kwenda Chuo kikuu moja kwa moja!? Mh, ngumu kumeza!
 
Kweli nimeamini watu wana upeo mdogo wa kufikiri, hata kusoma tu bila kufikiri bado hamuelewi?TCU hawajakosea chochote huu mfumo unatumika dunia nzima, mbona hao wanaosoma secondary na kuingia chuo hatuoni wanachokifanya?wanatoka vyuoni wanaajiriwa na watu walioishia std 7?wengine wamemaliza hata kiingereza hawajui kuongea sembuse kufanya mambo ya maana? Lengo hoa ni kumpa kila mmoja fursa ya kuendeleza alichonacho

kaka mi nakubaliana kidogo na wewe lakin mengine hapana!kwa mfumo wa elimu tulionao tanzania ni ngumu kwa std 7 kuanza chuo kikuu i.e vyuo vingi havitoi ujuz ila notisi nyingi,so bingwa wa kukariri ndo anaefaulu.serikali ingetoa fungu kuimarisha veta zitoe degree na hao std 7 wote wapitie veta na si kwingineko.
 
Aisee kutakuwa na shahada kibao! Kama Nigeria! Ngoja madiwani, waigizaji, wasanii, wapenda sifa n.k wapate hizi habari. Yaani katika hivyo vyuo kutakuwa na kurupushani kama mtaa wa Kongo pale sokoni Kariakoo; kila mtu akigombania shahada yake.
Sijajua kama hizo shahada zitatambulika hata hapo Kenya. Naona kama zitakuwa 'home schooling'. Wale mlio na ufahamu juu ya mifumo mbalimbali ya Elimu tunaomba ufafanuzi wenu katika hili.

Kazi itakuwa kubwa mbona.
Let us see, ila nimechekaa
 
Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:

“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”

Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.

“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Livingston Lusinde awe wa kwanza kujiunga Mzumbe
 
Back
Top Bottom