TCRA yawatoa hofu watumiaji wa laini moja

TCRA yawatoa hofu watumiaji wa laini moja

Majs

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
232
Reaction score
520
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaondolea hofu watumiaji wa mitandao ya simu, wanaotaka kutumia huduma ya laini moja kwa mitandao yote, kuwa hatawakosa huduma zinazotolewa na makampuni ya simu.

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Tehama wa mamlaka, Nehemia Mwenisongole, alisema hayo Jijini Arusha jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema huduma hiyo itakuwa ya hiari kwa watumiaji wa mitandao ya simu na itawasaidia kuondokana na kumiliki utitiri wa laini nyingi za simu na kutumia laini moja, iliyobeba mitandao yote ya simu ambayo atahitaji kutumia.

“Ukiamua kuhamia kwenye mfumo huu wa kuunganishwa kutumia namba moja, hakutakuwepo na madhara ya kuanza kuwaza kuwa wapo watu ambao nitawapoteza nikiingia huko,’’ alisema. Alisema kuingia kwenye mfumo huo, kutasaidia kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mtandao mahali mtumiaji atakapokuwa na kumsaidia kutumia mtandao mwingine.
 
Tatizo ili kuhama tena au kurudi mtandao wa mwanzo inachukua miezi, sikumbukuki vizuri lakini nadhani ni miezi 6 au 3
 
Sijaona umuhimu wa hiyo MNP nitabaki na simu yangu ya line 2 na line zangu mbili moja kama backup.
 
Back
Top Bottom