TCRA/TRA NA MAMLAKA YA LESENI KURUDISHA HESHIMA YA UFUNDI ILIYOPOTEA.

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
TCRA/TRA NA MAMLAKA YA LESENI KURUDISHA HESHIMA YA UFUNDI SIMU ILIYOPOTEA.


Kwanza napenda kutoa shukrani zangu kwa vitengo vilivyotajwa hapo juu pamoja na hayo, pia ujio wa muswada wa sheria hii ya kuondoa vitu feki nchini.

Madhumuni ya kuondoa takataka (simu feki) ni zoezi linalofanywa na TCRA baada ya kuona mbali na matatizo mbali mbali yatokanayo simu feki.

Simu feki zina madhara mengi kwa mtumiaji.

Madhara haya ni kama ifuatavyo:-

1. Simu feki zimeundwa kwa kemikali kali pamoja na mionzi ambayo ni mbaya kwa afya kwani hazizingatii viwango vilivyoweka kimataifa kutunza afya na mazingira kumlinda mtumiaji.


2. Betri zinazotumika kwenye simu hizi zinamadini ambayo yanatumika kutengeneza milipuko hivyo kuwa nayo ni sawa na kuishi na bomu, watumiaji wengi wamelipukiwa hasa wanawake ambao huweka simu hizo sehemu nyeti yenye joto kali. Mfano kwenye maziwa, hivyo hutengeneza joto ambalo uleta muwako na kuweza kulipuka. Kumbuka kila betri limepangiwa kiwango cha joto, betri original zimeandikwa joto 29 C.



3. Simu feki zimetengenezwa kwa chip dhaifu inaitwa Media Tech ki-iutaalam inaitwa MTK, chipset hii ni nyepesi sana kwa simu za android, kwani unaweza ku-edit unavyotaka, na chip hii ndio inayouzwa bei ndogo kuliko chip nyingine kama MTK, Qualcomm, Broadcom, Hi-Silicon and TI OMAP , na n.k. Hivyo ni rahisi kwa mtu yeyote kuweza kuihujumu anayvotaka kutoka huhalisia kama kubadili software, ku-edit imei. Kampuni nyingi huzikimbilia hili ziwe nafuu kwao lakini hazina security protection za kutosha. Mfano. Samsung ina chip ya QUALCOMM si rahisi kutoa FRP yaani Factory Reset Protection mpaka upate au uombe kutolewa security kwao. Wakati MTK ni on the sport kwani unaweza ku-Erase Simu yote ikawa empty body n ku-rod upya ikwa mwonekano mwingine.


4. Simu feki huzimika wakati wowote na fundi asiweze kuifufua kwa kuwa watengenezaji wanadanganya sana firmware walizoziweka, unaweza ukazani ni MTK Alps kumbe ni Samsung, hivyo huleta mfarakano kati ya mafundi na wateja.



5. Simu feki hutumiwa sana na watu wenye nia mbaya kama majambazi kwani wanaweza kubadili imei yoyote bila kuwasiliana na fundi , kuna komand Fulani ambayo kwa kutumia simu unaweza kuiping ikakuretea engineer mode ambayo unaweza kubadilisha imei unavyotaka bila kutumia computer wala apps za simu hivyo kuharibu utambulisho wa simu

6. Simu feki hazina spare specific kwani watengenezaji kwa kuwa ni wengi, huweza kuweka kila kinachoonekana kumpendeza mteja, bila kuweka rebal ya product,au udaganya kwa kuweka lebel feki hivyo utengenezwa kwa kubahatisha, mfano Samsung i9500 na n910 imebadilishwa mara tatu, hivyo huitaji kutumia gharama kubwa kudownload mafile mengi ili kupata iliyo sahihi.

Napenda kuanza na historia ya simu ili kuweka kumbukumbu sahihi kwa waanzilishi wa secta hii muhimu ambayo imekuja kutoa ajira kwa vijana zaidi ya laki tatu

Mtu wa kwanza kuanza kutengeneza simu ni Peter Lema ambaye alikuwa mfanyakazi wa Tritel , ambaye aliajiriwa Tritel kutoka chuo cha Dar Tech kama fundi wa kurekebisha simudigital, huyu alikuwa akishirikiana na Mafundi wa bobezi waliokuwa wanafundisha Dar Tech, ambao ni Mkude na Mwalembe ambao baadaye walifungua chuo kariakoo na kampuni yao ikiitwa YOWIFO.

Mwanzilishi Peter Lema alilewa sifa kutokana na upatikanaji wa pesa nyingi akawa na kundi kubwa la vijana ambao walimfundisha starehe sana akashindwa kuwahudumia wateja. Vijana hawa (majina kapuni) walimwalibia sana sifa ikaonekana kuwa ufundi huu ni sehemu ya uhuni, jambo ambalo lilimfanya akimbie mji kujinusuru na marafiki wabaya ndipo akaenda Arusha na Moshi, bila kumungunya maneno, kijana mwenye asili ya KinyarwandaAbdul, alikuwa ni mwizi balaa, alikuwa akimwibia simu za wateja na kumfanya kila siku kesi polisi.

Kuibuka kwa vijana wapya ambao waliweza kuiweka gsm industry kwenye mwelekeo sahihi walikuwa ni Mwesiga , Yahyana sele ambao waliweza kujenga ofisi za kudumu na kupatikana kiurahisi pamoja na kusajili ofisi zao kisheria. Kundi la Pili wakaja John Ndembwike, Abdala Maige , Mganda Gasta Birungi, wakaunda kampuni yao ya ushindani, kipindi hicho Tanzania mzima simu zote zilikuwa zinatengenezwa posta tu. Wakaja kundi la tatu, ambao walikuwa wamebobea kwenye hardware, chiba, Sele, Dula sheshe, Dula Bonge, Mengi na kuzacha. Kundi la nne wakaja Munna mtaa wa India, Naimu pale mnazi mmoja.

Kundi linguine likaja la vijana matapeli ambao walitengeneza vibao vingi na kuvibandika mbele ya viosk au meza zao za kutengeneza simu, kundi ili lilifanya uhribifu na uharifu mkubwa sana kiasi kwamba kituo cha polisi Msimbazi kwa siku walikuwa wakipokea kesi zaidi ya kumi za uharibifu. Kundi hili liliharibu tswira ya ufundi simu na kuonekana ni ajira ya kihuni. Kuanzia hapo uhaminifu kwa mafundi simu dhidi ya mteja ukafa, ili utengeneze simu ikawa kwamba ni lazima mteja akae pale pale akikukagua na kukuangalia eti usimwibie utumbo. Kundi iliongezeka sana na kutengeneza meza nyingi kila kona, na kundi hilo pia liliweza kuharibu soko la kutengeneza simu .

Kwa nini napongeza ujio wa TCRA, TRA na Mamlaka ya leseni kwa uhamuzi wao wa kwamba ili uwe fundi simu unayetambulika ni lazima ujisajiri kisheria ufuate taratibu zote ikiwa na kuwa na cheti cha mafunzo VETA ni kwamba itaondoa mafundi feki wasio na taaluma, itaondoa madalali waliojibanza vibalazani kusubiri wateja wa kuwadanganya, itaondoa mashaka ya wateja kuibiwa vifaa vyao vya ndani, itaongeza ufanisi kwani mteja anakutana na mtu sahihi. Itapunguza kesi nyingi polisi kwani mteja ataweza kupata haki zake za msingi pia hata mtengenezaji.

Hii dhana imeamusha vyuo kwa sasa , VETA itaajiri walimu wa fani hii adimu na kudaili wanafunzi wengi wanaopenda fani hii kuipata kwa wepesi kwani wengi walikuwa wakijifunza kihorela, hawajuhi basic electronic need. Hivyo ita-wabust kuingia kwenye soko la ajira kwa wale wote wanaotaka kuingia mikataba ya kufungua makambuni ya kuhudumi simu. Mfano, Tecno, Huwei, Samsung, Nokia watapata wataalam wa kuhudumia simu zao kwa njia hii.Pia itawaongezea uwezo wa kudadisi technologia mpya, mfano sasa hivi tuna simu za 4g ambazo ni complicated sana.

Maombi kwa serikali,Serikali hii ya Magufuri ya Hapa kazi tu, sekta hii ishakuwa ajira, secta hii kwenye katiba haipo kabisa, haikupata wawakilishi kutoa maoni yao, safari hii katiba itakaporudiwa tunaomba kutoa maoni ambayo yatatungiwa sheria ya kulinda mafundi na kulinda mteja kwani polisi wanamanyanyaso sana, kuliko kuiacha kiohorera kwani ni chanzo cha kuchangia uchumi.

Mwisho kabisa naomba TCRA, TRA, na Mamlaka ya Leseni kuahakisha kuwa inafanya ukaguzi wa kina kubaini mafundi waharibifu, pia wasiokidhi viwango vya taaluma ili kulinda masirahi mapana ya mtumiaji, ili kuondoa dhana ya mafundi kutoaminika kwa wateja wao. TRA kukutana na wadau kuwasikiliza matatizo yao yanayoendana na tozo za kodi kwani kodi iliyopo ni ya unyanyasaji, kwa kuwa hawajui kipato halisi cha ufundi huu
 
ClSQI35WAAAib9V.jpg
 
Umenifanya nicheke.

Ila hii pia ni kama ile ya kuhamishia mizigo kupitia bandari ya Beira,Durban au Mombasa baada ya serikali ya Dar es Salaam kuwa na masharti yasiyo rafiki kwao...
Kha! untka kukimbilia jirani?
 
Hehehe watu wamekosa kazi duh!
Tanzania miaka kumi mbele mtakua mnaimba wimbo huu huu, hadi pale vila.za wote watakapopotea waache nchi iongozwe na watu smart.
 
Siwezi kukimbilia jirani. Kwa jirani machafuko kila siku.

Napenda kwetu kuwe na fursa nzuri na rafiki kwa wafanyabiashara ili wasitamani kwenda kwa jirani...
 
Hehehe watu wamekosa kazi duh!
Tanzania miaka kumi mbele mtakua mnaimba wimbo huu huu, hadi pale vila.za wote watakapopotea waache nchi iongozwe na watu smart.
serikali hii ya magufuri haitaji vila.za hata wafagiaji wa barabarani wanatakiwa wawe na elimu ya form four, ili wajue jinsi ya kujikinga na vumbi, uchafu dhidi ya bakitelia, la saba watabaki kubeba mizigo mizito nao baadaye wataktaliwa kwani ni lazima wajue vipimo vya afya zao na kiwango cha body zao kwa mizigo husika
 
serikali hii ya magufuri haitaji vila.za hata wafagiaji wa barabarani wanatakiwa wawe na elimu ya form four, ili wajue jinsi ya kujikinga na vumbi, uchafu dhidi ya bakitelia, la saba watabaki kubeba mizigo mizito nao baadaye wataktaliwa kwani ni lazima wajue vipimo vya afya zao na kiwango cha body zao kwa mizigo husika

Naona umesahau kuna mkuu wa wilaya alikua anaapishwa hata kusoma alikua hajui. Tusijidanganye kua kuna kipya wakati ukweli ni kua tunafanya marudio.
 
Naona umesahau kuna mkuu wa wilaya alikua anaapishwa hata kusoma alikua hajui. Tusijidanganye kua kuna kipya wakati ukweli ni kua tunafanya marudio.
Hata Dr. tulia alishindwa kujieleza lakini alipita kwa figisu figisu
 
Back
Top Bottom