Kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania pia ni uzembe wa serikali kwa kuto structure uchumi vizuri. Na hii imetokana na high importation ya products from western than exportation of our products. Tunapoagiza au kununua bidhaa yoyote toka nje mara nyingi tunalipa/tunatozwa kwa dollar. Hii inafanya serikali itafute dollar za kutosha ili kuweza kufanya manunuzi (procurement) nje ya nchi.
Kumbuka pia theory isemayo; "The higher the demand, the higher the price" Kupanda kwa dollar pia kunatokana na pesa hiyo kuhitajika kwa wingi kama almas katika sehem nyingi katika malipo km vile kwenye maduka makubwa, mahotelini, na kwenye makampuni mbalimbali.
Kama serikali ingekuwa makini kwa kuweka sheria kuwa malipo yote Tanzania yalipwe kwa Tshs nadhan shilingi isingeporomoka kwa kiasi kikubwa namna hii coz ingekuwa "high demanded" kitu ambacho kingeongeza thamani yake. Sasa hiv ni jambo la kawaida ukiingia kwenye baadhi ya mahoteli makubwa ukakuta malipo yanafanyika kwa dollar. Si mahoteli tu bali hata masuper markets makubwa baadhi yanataka malipo kwa dollar. Kwa mfumo huo ni lazima shilingi ishuke thamani tu!
TCRA ni mbwa asiyebweka na hakuna kazi wanayoifanya zaidi ya kutafuna mishahara na kuongeza vitambi vyao. Ningekuwa nina mamlaka ningevunja TCRA na kuunda chombo kingine ambacho kingepigania haki ya msingi ya watanzania ya mawasiliano. Walikuja kasi na ujenzi wa mkonge wa wa mawasiliano lakini sasahiv wamekuwa kimya tu sijui hata wameishia wapi. Kampuni ya TTCL nayo haikui sijui ndo njama zao TCRA ili makampuni ya simu za mkononi yaendelee kujipatia mahela ya bure bure kutoka kwa watanzania?