Mnyalu Junior
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 573
- 200
Ni jambo lisilopingika na linalofahamika wazi kwamba huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Ni mara nyingi pia unaweza sikia usemi usemao: Sasa hivi dunia ni kama kijiji.
Kukua kwa teknolojia ya kupashana habari ulimwenguni kumeleta urahisi mkubwa kwa watu kujua mambo mbalimbali yaliyopo na yanayoendelea hapa duniani.
Back to the Topic:
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) ni mamlaka iliyowekwa na yenye wajibu kisheria kusimamia masuala yote yahusuyo mawasiliano nchini Tanzania.
Cha kushangaza mamlaka hii imekuwa kimya kwa sintofahamu nyingi zinazohusu mamlaka hiyo. Kuna mambo mengi ambayo binafsi naona mamlaka hii imeshindwa kazi kama vile:
SUALA LA VING'AMUZI
Wakati wanahamasisha mchakato wa kuondoka kwenye mfumo wa analogia na kuingia mfumo wa digitali walitamka wazi ya kwamba chaneli zote za ndani ya nchi (Local Channels) zitawekwa katika ving'amuzi hivyo na zitaoneshwa bure. Chaneli za ziada ndizo zitalipiwa.
Lakini imekuwa kinyume kabisa. Kuna makampuni ya ving'amuzi yaliyowekeza hapa Tanania kama: DSTV, TING, ZUKU, AZAM, CONTINENTAL, nk ambayo kama hujalipia hata kwa vifurushi vyao vya hali ya chini basi huwezi pata chaneli hata moja ya kitanzania!
GHARAMA ZA MITANDAO YA SIMU
Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la gharama za simu pasipo taarifa kwa watumiaji wa simu za mkononi. Watu wengi tulilalamika kuhusu hili lakini wao waliweka pamba masikioni. Sijui wanagawiwaga 10%? Gharama hiyo imekuwa kubwa sana hasa kwa bando za intaneti, kwa mfano mtandao wa Vodacom hata uunge kifurushi chochote cha dakika cha siku umekuwa ukitoa MB 8 pekee!
Baadhi ya viongozi kama Januari Makamba walijifanya kusikitishwa na suala hili na wakaahidi watalishughulikia lakini imekuwa kimya. Sijui tuseme ulikuwa ni unafiki tu??
TCRA kazi imewashinda na mnafaa mlaumiwe kwa kuwabebesha watanzania wa kipato cha chini kama mimi mzigo mkubwa wa gharama kubwa za mawasiliano.
Ukitaka kujua kuwa hawa TCRA ni wanafiki na hawatekelezi majukumu yao kama walivyoainisha soma hapa:
Tovuti Kuu ya Serikali: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania