TCRA, kampuni za Google, Facebook, Whatsapp, Instagram zakwepa kodi ya mabilioni Tanzania

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Kampuni kubwa za Google, Facebook, WhatsApp, Instagram zimekuwa zikifanya kazi bila ya usajili wala kulipa kodi kutokana na uzembe wa mamlaka ya TCRA, aidha kwa makusudi au TCRA kutojua namna ya kuzitoza kodi.

Ukinunua simu unakuta Google ishakuwa installed.

Nchi kama China kutokana na Facebook kukwepa kodi imezuiliwa software yake na shirika la kijasusi kutofanya kazi nchi ya China. Hata ukiwa na simu huwezi pata access ya kuchat kutumia facebook.

Lakini Tanzania haya mashirika makubwa yamekuwa yakijizolea pesa za kumwaga bila ya kusajiliwa.

Ukiangalia TCRA hawana kitengo kama Brella cha kusajili application software ,social networks.
Wameshindwa kutengeneza filter ya kuzuia social networks zisizolipa kodi kuoperate nchini.

Kuliko kuwatoza hawa maskini fedha za kingamuzi naomba wafungue kesi kuzishitaki kampuni hizi kuwa kufanya kazi kinyemela bila kibali cha serikali.

29STEWART-master768.jpg
 
Sasa watozwe kodi kwa lipi????
Pili facebook hawajafungiwa sababu ya kodi ila ni sababu serikali yao ina sheria za kubana uhuru wa habari na fb waligoma kukubaliana na matakwa ya serikali, fanya utafiti kabla ya kudanganya watu
 
Kwani wewe tangua uanze kutumia Facebook Au Watsapp au Instagram umeshalipia sh ngapi? So kama facebook wanalipwa na Toyota ya Japan kutangaza biashara zao hao wa Japan ndio watapata Vat n.k
Kwa kweli suala la TZ kudai kodi kwenye mitandao bado ni gumu sana na inahitaji kuja na concrete reason ya jinsi ya kupata kodi...
 
Hiki ni kituko cha kwanza nimeona leo.
We unataka Facebook na Whatsapp walipe kodi Tanzania? Hehehe kwani wanaoperate nchini?
China hawajawafungia kwa kua hawalipi kodi, wamewafungia sababu hawana demokrasia, uwepo wa Facebook au Google ambayo haiko filtered unahatarisha serikali yao ya ki~communist. Google ipo china ila inakua filtered.

Huwezi kucharge kampuni kama Facebook nchini sababu tu wana website unayoweza kuiaccess, kuna website nyingi utadhani population ya Africa nzima, utazilipisha zote kodi? Kampuni yoyote ile inayooperate online kama hawana ofisi nchini kwako sahau kuhusu kodi.
 
Ama kweli hii nchi sio maskini mkuu.. Kwamba unataka kuniambia kuanzia Google, Facebook, whatsapp, applications na mitandao mingine ilikua inaoperate free of charge hapa Tz?
 
Hehe whatsapp walipe kodi Tanzania? Mkuu sisi tushukuru tu whatsapp na facebook hawajafunga huduma zao Africa. Bado unataka wakulipe kodi? Yaani wakupe huduma ya bure na bado wakulipe. Hao wachina wameifungia facebook ili kunyima uhuru wa habar kwa wananchi hii ya kodi ndo naisikia leo.
 
Kuiga siyo mbaya lakini ni kama mapema sana hata tunaye muiga bado hojazake hajaziweka sawa.
Tushukuru kwa kulileta hili nasi tuchungulie walioanza na hoja zao.
 
Hivi Ofisi zao hapo Tanzania ziko wapi vile
Ama kweli hii nchi sio maskini mkuu.. Kwamba unataka kuniambia kuanzia Google, Facebook, whatsapp, applications na mitandao mingine ilikua inaoperate free of charge hapa Tz?

Hivi Ofisi zao hapo Tanzania ziko mkoa gani vile.
 
Google wana ofisi Tanzania?

Tanzania imeshindwa kuwalipisha kodi raia wake itaweza kuilipisha kodi kampuni ambayo haina ofisi wala kuuza bidhaa Tanzania?
 
Google wana ofisi Tanzania?

Tanzania imeshindwa kuwalipidha kodi raia wake itaweza kuilipisha kodi kampuni ambayo haina ofisi wala kuuza bidhaa Tanzania?
UNAITUMIAJE HII SEARCH ENGINE KAMA HAIPO TANZANIA??
KWA MAANA HIYO INAOPERATE KINYEMELA , IZIMWE KWENYE GATEWAY YA NCHI ; NA SATELLITE WAWEKE FILTTER YA KUIZUIA .
MPK IFANYE TARATIBU ZA KUJISAJILI TCRA.
MFANO WA KUTOISAJILI NI JINSI WALIVYOITUMIA KUDHIAKI JK KIPINDI KILE KWA PICHA MBOVU
 
Search engine ipo kwenye servers zao, ambazo hazipo Tanzania.

Wewe unayetumia servers zao ndiye unayetakiwa kuwalipa.

Kama hutaki acha. Hawajakulazimisha.

Kuna vitu elfu moja na moja vya kutoza kodi. Kwa nini uanzie na vya kufikirika tu?
 
NANI AMBAE HALIPI??
SIMU KAMA HAINA KIFURUSHI FUNGUA GOOGLE KAMA HUTAIPATA?
KWANINI UKIWEKA PESA NDO UNAIPATA , TENA UKIACHA DATA ON.

NDO HUJUE KUWA JAMAA WANACHUMA MPK KWA WATU MASIKINI.
 
Hiki ni kituko cha kwanza nimeona leo.
We unataka Facebook na Whatsapp walipe kodi Tanzania? Hehehe kwani wanaoperate nchini?
China hawajawafungia kwa kua hawalipi kodi, wamewafungia sababu hawana demokrasia, uwepo wa Facebook au Google ambayo haiko filtered unahatarisha serikali yao ya ki~communist. Google ipo china ila inakua filtered.

Huwezi kucharge kampuni kama Facebook nchini sababu tu wana website unayoweza kuiaccess, kuna website nyingi utadhani population ya Africa nzima, utazilipisha zote kodi? Kampuni yoyote ile inayooperate online kama hawana ofisi nchini kwako sahau kuhusu kodi.
Well said. Vilaza wengi humu JF.
 
NANI AMBAE HALIPI??
SIMU KAMA HAINA KIFURUSHI FUNGUA GOOGLE KAMA HUTAIPATA?
KWANINI UKIWEKA PESA NDO UNAIPATA , TENA UKIACHA DATA ON.

NDO HUJUE KUWA JAMAA WANACHUMA MPK KWA WATU MASIKINI.

Mkali mawazo yako yana nipinguzia stress sana.
Hii hoja inahitaji urudi ubaoni, ni Kama umekurupuka hivi rudi kaisome vizuri halafu ndio tuhojiane zaidi.
 
Back
Top Bottom