TCRA badilisheni huo utaratibu mnaotaka

TCRA badilisheni huo utaratibu mnaotaka

fdizzle

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
1,902
Reaction score
2,405
Huu utaratibu mpya wa kujisajili upya tena kwa kitambulisho kimoja tu cha taifa ni janga.

Tatizo sio hizo finger prints tatizo Ni aina ya kitambulisho kinachotakiwa. Kama nia yenu ni kuongeza mapato kwa zile 100/= za meseji za kupata namba ya kitambulisho basi kwa mfumo huo ni sawa.

Lakini Kama mna nia ya kuhakikisha watu wanapata huduma nzuri ya mawasiliano pamoja na kudhibiti uhalifu basi ongezeni na vitambulisho vingine ili wengi wapate kujisajili.

Tutegemee yafuatayo endapo kitatumika kitambulisho kimoja cha taifa:

Kwanza kupungua kwa idadi ya watumiaji wa simu ya mkononi. Hii ni kwa kuwa wengi wao hawana hivyo vitambulisho vya taifa.

Kwa mfano katika mtaa niliopo kati ya watu kumi ni mmoja ndie nwenye kitambulisho. Pili, hili litapelekea kupanda kwa bei ya line za simu aidha kwa wafanyakazi wa kampuni za simu kutengeneza line na kuziuza kwa bei kubwa si ajabu line kuuzwa kwa elfu 50 na watu watanunua tu matokeo yake mtakuja na tamko lingine.

Kukosekana kwa ajira kwa mawakala wa kusajili line kwa kuwa si wote watakaonudu kununua vifaa vya kuchukulia finger print.

Kuikosesha serikali mapato kutokana na kupungua kwa watumiaji wa vocha
Kupoteza nguvu kazi kwa watu kushinda kwenye foleni za kusubiri kujisajili
Ushauri wangu kwenu ongezen idadi ya vitambulisho vya kujisajilia
 
Najiuliza tu huku mpitimbi niliko mm hata gari halifiki nauli kwenda mjn kufuata hyo huduma n gharama kubwa vitambulisho vya taifa toka tujiandkishe mwaka Jana mwez wa tano na sasa unakaribia mwaka hatujapata sielew sjui hii SIRI-KALI inataka nn najiuliza tu tuna utitiri wa vtambulisho tungeweza tumia kmojawapo kakuwa wanasiasa kitambulisho cha taifa sio muhimu kwao ila cha mpiga kura wangehakikisha kila mmoja anakipata kwa gharama yeyote
 
Mliipenda wenyewe,tuliwaambia CCM ni ile ile.

Hata aje nani kile Chama hakina mawazo mbadala.

Wao ni Kumuongezea Mwananchi Mzigo kila sehemu.
 
Sijui walifikiria nini hawa jamaa
Najiuliza tu huku mpitimbi niliko mm hata gari halifiki nauli kwenda mjn kufuata hyo huduma n gharama kubwa vitambulisho vya taifa toka tujiandkishe mwaka Jana mwez wa tano na sasa unakaribia mwaka hatujapata sielew sjui hii SIRI-KALI inataka nn najiuliza tu tuna utitiri wa vtambulisho tungeweza tumia kmojawapo kakuwa wanasiasa kitambulisho cha taifa sio muhimu kwao ila cha mpiga kura wangehakikisha kila mmoja anakipata kwa gharama yeyote
 
Hii habari ya kila mara tunajisajili ni upuuzi na kupoteza muda kama hakuna plan ya muda mrefu kaaeni kimya .
Kama mnaona hiyo ni issue ya lazima wekeni vitambulisho vingi na wakala wengi mabenki , kampuni za simu , TRA, hospitali ili watu wasipiteze muda kuweka hizo finger print
 
Ila nilishasemaga, jamani msione tupo kimya, kuna kitu tunataka kuja nacho kitakachobadilisha upepo wa kuzungumzia issue ya CAG, sasa kuanzia May Mosi usajli wa simu card kutumia kitambuisho cha taifa ndiyo ita trend...

Hiyo inaitwa funika kombe.... .... apite...


Hili la kupungua kwa watumiaji wa simu wala siyo la kuuliza lazima litokee...



Cc: mahondaw
 
Nimetenga Tsh elfu 50 kununua line iliyosajiliwa na kitambulisho cha NIDA. NIMEAPA kutokanyaga nida kuchukua ID na wala kupanga foleni kusajili line. This time, money will talk.
 
Back
Top Bottom