singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
CHAMA cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kimesema kamwe hakitawatetea wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi, hivyo kimewataka wanachama wake kuhakikisha wanatii sheria za nchi, ikiwemo kulipa kodi stahiki kwa serikali.
Akizungumza jana kuhusu kufanyika kwa mkutano wa wanachama wa TCCIA kesho jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dar es Salaam, Francis Lukwaro alisema chama kimekuwa kinawahamasisha wanachama wake walipe kodi ili waisaidie nchi katika kuinua uchumi wake.
“Katika mkutano wetu wa Ijumaa (kesho), tutajadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati alipokutana na wafanyabiashara, miongoni mwa masuala tutakayoyajadili ni hilo suala ukwepaji kodi ambalo ni moja ya ajenda zetu,” alieleza Lukwaro.
Lukwaro alisema madhumuni ya mkutano huo ni kujadili mwelekeo wa sekta binafsi katika kuunga mkono jitihada katika kuboresha mazingira ya biashara na kukuza uchumi wa nchi.
Alisema wanachama wa TCCIA watatoa michango yao ya namna ya kuboresha mazingira ya biashara ili sekta binafsi itoe mchango unaostahili katika ujenzi wa uchumi wa nchi na kwa manufaa ya wananchi walio wengi.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ndiye atakuwa mgeni rasmi wa mkutano huo ambao utawashirikisha wafanyabiashara wapatao 300 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam.
Mikoa mingine nayo itafanya mikutano ya namna hiyo kujadili hotuba hiyo ya Rais Magufuli.
Lukwaro alisema maeneo ambayo wanachama na wafanyabiashara watatoa mapendekezo yao ni kuhusu sheria na taratibu ambazo zikiboreshwa kutaongeza faida na kukuza biashara na shughuli zao za kiuchumi.
Eneo lingine ambalo litajadiliwa ni sekta binafsi inawezaje kuchangia kuongeza mapato ya Serikali na pia watashauri juu ya fursa za uwekezaji zilizodokezwa na Dk Magufuli kwa wafanyabiashara wakati alipozungumza nao mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Last edited by a moderator: