TBS kagueni ubora wa dawa ya Whitedent

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
5,210
4,172
index.jpeg


Ni ombi langu kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufanya utafiti juu ya dawa ya meno Whitedent, maana imekuwa tatizo kwa watumiaji, hasa kwenye eneo la lips. Watumiaji hupata mipasuko katika eneo hilo.

Yamkini yawezekana kuna kemikali; aidha wamezidisha, au wamepunguza.

Naomba kuwasilisha.
 
hata ukichunguza kwa undani utagundua pindi unapoitumia, kuhisi kuungua kwa lips yako.

Baada ya hapo utaona midomo inaanza kukauka na kupasuka.

Hili tbs ilichunguze jamani maana umagumashi, utagharimu Afya za watu jamani.

Maana magonjwa yanaliandama taifa hili kutokana baadhi ya watu kuchakachua bidhaa.
 
Sio TBS tu,na TFDA pia.Taasisi nyingi za Umma ni JANGA LA KITAIFA.Na ndio maana saratani imeota mizizi nchini kwa kubugia sumu huku wenye wajibu wao 'wanabembea' kwenye viti maofisini huku wakipulizwa na viyoyozi na 'shangingi' lenye 4WD likimsubiri nje.Halafu Magufuli akiwatimua wanasema ni dikteta!! Hovyo kabisa!
 
Sio TBS tu,na TFDA pia.Taasisi nyingi za Umma ni JANGA LA KITAIFA.Na ndio maana saratani imeota mizizi nchini kwa kubugia sumu huku wenye wajibu wao 'wanabembea' kwenye viti maofisini huku wakipulizwa na viyoyozi na 'shangingi' lenye 4WD likimsubiri nje.Halafu Magufuli akiwatimua wanasema ni dikteta!! Hovyo kabisa!
mimi nafikiri kwenye izi taasisi kuna vidonda ndugu kabisa siyo tena majipu.

Nakuunga mkono mkuu kwa sababu taifa lina Angamia kwa magonjwa ya nayosababishwa na uzembe wa izi taasisi 2.
 
Kama ni sumu tumeshakula sana. Lakini cha ajabu huko TFDA na TBS ndio miongoni wanaolipa mishahara minono mno.
 
Hata colgate now zipo ambazo si sahihi na za kiwango cha chini. Ukitaka kujua Colgate ni fake na ya magumashi.......tazama box......kama box lake milango yake imewekewa gundi yaani si ya kufungua na kurudishia basi jua hiyo si Colgate halisi wametumia majina tu ila ni wahuni.......hizi colgate za magumashi zimesambaa sana huku uswazi na kwenye maduka mengi.....kama utaona ni risk sana nakushauri nunua dawa za gharama lakini zenye ubora mimi natumia alovera ya forever living.....ila nataka nitafute na brand nyinginezo ambazo nitakuwa na uhakika wa usalama wa hizo product.
 
View attachment 346366

Ni ombi langu kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufanya utafiti juu ya dawa ya meno Whitedent, maana imekuwa tatizo kwa watumiaji, hasa kwenye eneo la lips. Watumiaji hupata mipasuko katika eneo hilo.

Yumkini yawezekana kuna kemikali; aidha wamezidisha, au wamepunguza.

Naomba kuwasilisha.
mkuu nikueleze tu kuwa TBS hawawezi kuwafanya kitu hao whitedent, narudia tena TBS ilishashikwa masikio na whitedent. ubora wa dawa zao hapa nchini upo chini ya viwango na na tbs wanalijua hilo. Profesa EN Kikwilu wa MUHAS SCHOOL OF DENTISTRY aliwahi kufanya utafiti wa ubora wa dawa za meno zinazo uzwa kwenye soko la tanzania kwa kuangalia fluoride content (fluoride ni ingredient inayo zuia meno kutoboka) na ili fluoride ilete matokeo yanayo kusudiwa inatakiwa kuwa na concentration isiyopungua 1000ppm( parts per milion). matokeo ya profesa kikwilu yalionesha kuwa whitedent ina fluoride chini ya 1000ppm!!! na hivyo haitoi ulinzi kamili wa meno kama wanavyo tangaza kwenye vyombo vya habari. matokeo ya utafiti huo TBS inao
Dawa za meno nyingine zilizo husishwa kwenye utafiti huo ni Colgate na Aha ambazo zilionekana kuwa na kiwango sahihi cha fluoride. Baada ya utafiti huo kuonesha whitedent ina fluoride chini ya kiwango tofauti na colgate na aha, dawa ya aha ilipotea sokoni na haijawahi kuonekana tena (nini kilimkuta huyo mzalishaji wa bidhaa bora mpaka akapotea sokoni?.........)
kwahiyo ndugu yangu unapo question ubora wa whitedent binafsi nakuelewa sana, mzalishaji wa whitedent anatafuta faida ya juu kwa kupunguza ubora wa bidhaa yake.
 
Dawa nyingi za meno ni za kufuatiliwa na taasisi husika kama TFDA na TBS. Niliwahi kununua dawa ya Sensodyne kutoka kwenye pharmacy moja kwa 7,000/= nikaona dawa iko vizuri tu. Baadae nikakuta dawa za aina hiyo ujazo huo huo zinauzwa pharmacy nyingine tofauti kwa 5,000/= kila tube. Kwa kuona unafuu wa bei nikanunua tube 4. Nilipofika nyumbani na kufungua moja nikagundua ina ladha tofauti kabisa na kwa ujumla ilikuwa fake kwa sababu hata seal yake kwenye tube ilikuwa ni ya kubandika kijuujuu tu tofauti na ile niliyokuwa nimenunua awali.

Nilijaribu kuwapigia simu TFDA na kuwaeleza mkasa huo lakini wakawa wanatupiana mpira na TBS nami nikakosa muda zaidi wa kufuatilia.
 
Sasa mnanunua kwa mtutu wa bunduki ?
Dawa zao zina ubora wa chini na ni bei ndogo, pia wamedominate soko la dawa za meno hapa nchini huku waki danganya mtumiaji kwa kuzipachika dawa zao ubora zisizo kuwa nao, kilicho andikwa juu sicho kilichomo kwenye dawa.
 
Back
Top Bottom