TBC ndio kielelezo cha Ustawi wa Taifa

TBC ndio kielelezo cha Ustawi wa Taifa

Joined
Jul 8, 2013
Posts
54
Reaction score
76
Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Mei mwaka huu litatimiza miaka 70 ya Uhai wake.

TBC uliasisiwa mwaka 1951 na wakati huo ilijulikana kama Sauti ya Dar es Salaam.

Tangu hapo TBC imepita vipindi mbalimbali na kubwa mojawapo likiwa ni kusaidia ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, ustawi wa Taifa na watu wake na kulinda utamaduni wa Taifa letu.

Kwa sasa TBC inamiliki vyombo vifuatavyo TBC 1, TBC 2, Safari Channel, TBC Taifa, TBC FM, TBC International na TBC Arusha.

Waandishi mahiri wa habari wanaofahamika ndani na nje ya nchi pia wamepikwa na shirika la Utangazaji la Taifa mfano Eda Sanga, Paul Sozigwa na wengineo.

Hakika TBC itaendelea kusalia kuwa Mama wa Utangazaji nchini.
 
Hivi wafanyakazi wa hilo shirika wana umri wa miaka mingapi.? Mana kuna baadhi ya vitu nikiangalia hua nashangaa sana, najiuliza hv kuna vijana kweli pale?
 
Hawana lolote zaidi ya propaganda, habari zetu zote google, youtube, insta, wasafi, jamiiforums etc... TBC waishie
 
Hakuna redio na TV station ya ovyo kama hiyo TBC... propaganda tupu na maslahi ya mafisadi wa CCM, waache kujiita kituo cha Taifa ni dharau mbaya sana kwa watanzania
 
Haina sifa ya kuitwa Television ya Taifa!

Television ya ccm
 
Back
Top Bottom