TBC mna bifu gani na CHADEMA?

TBC mna bifu gani na CHADEMA?

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
5,342
Reaction score
2,528
......Leo kwenye kipindi chao kinachorushwa kuanzia saa saba mchana kinachoitwa Dira ya mchana,TBC1 wametangaza habari ambayo naweza sema kuwa ni propaganda chafu zinazotumiwa na CCM kudhoofisha nguvu ya vyama vya upinzania hasa CHADEMA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kule Arumeru Mashariki.

......Akiripoti mwandishi wao amedai kuwa kuna wanachama wa CHADEMA na TLP wamejiunga CCM akiwepo M/kiti wa jumuiya ya wazazi wa TLP..cha kushangaza huyu mwandishi ameonyesha kadi ameonyesha kadi zisizopungua 10 za TLP na KUSHINDWA KABISA KUTUONYESHA KADI ZA WANACHAMA WA CHADEMA..Hii naweza sema ni mchezo mchafu na wakitoto tena unaorushwa na kituo chenye dhamana ya kulinda maslahi ya UMMA bila kulalia upande mmoja...napata taabu kufikiri kuwa mbona huyu mwandishi akutoonyesha kadi za CHADEMA? na mtu atahitwaje mwanachama wa CHADEMA bila kuwa na kadi?

......Ombi langu kwa chumba cha habari TBC1 wanapaswa kujua kuwa habari zao tunazisoma na kuzisikiliza na kuziona..utumbo wanaofanya kuna siku utawagharimu..na niwakati wa hawa waandishi wa hiki kituo cha habari kuzingatia weledi badala ya kuendelea kulalia CCM utadhani kuwa CCM watatawala milele.
 
Vita itakapotokea ya kuwang'oa CCM madarakani kwa nguvu hiki kituo kitakuwa cha kwanza kulipuliwa na wananchi.
 
kaka wala usijali wale watu wote wanaotaka mabadiliko na ambao ndio tunawategemea kukipa kura chadema wameshapuuza hyo TBC1 siku hizi. Vijana wote wenye upeo mpana ambao ndio mtaji wa chadema wanaangalia channel zenye kutoa elimu inayokwenda na wakati na wala sio hiyo tv inayotangaza kwamba taifa letu ni changa na vijana ni taifa la kesho.
 
Kwa nini ukilipue? Wanalazimishwa tu wale masikini wa watu na njaa zao.

Ukishaondoa tu Mkoloni Mweusi, na wao watabadilika hata bila kuambiwa.

Vita itakapotokea ya kuwang'oa CCM madarakani kwa nguvu hiki kituo kitakuwa cha kwanza kulipuliwa na wananchi.
 
Vita itakapotokea ya kuwang'oa CCM madarakani kwa nguvu hiki kituo kitakuwa cha kwanza kulipuliwa na wananchi.

Ndo maana Mkapa aliwakebehi hawa waandishi wa habari wa Kitanzania!full ubabaishaji,kujipendekeza na kutojua maadili ya taaluma zao,Tiddo Mhando was a right guy for Tbc,alikua anajua nini cha kufanya kutokana na taaluma yako,sio kupangiwa na kuambiwa la kufanya na watu wasio na taaluma
 
Yule mzinzi aliyekamatwa kule Igunga sijui anaitwa mwagala, watu wa Arumeru kuweni naye macho.Huyu penye haki na usawa yeye anaingiza rushwa kwa kugawa pesa,kununua kadi za kupigia kura,mawakala wake ni baadhi ya MaDC/watendaji katika serikali wasiowaaminifu, keshawakatia mgawo hao wanachama wa TLP ili kuyapa support magamba
 
achana nayo hiyo tbc1,kazi kubwa umbeya tu.lini utakuta cnn au bbc wanaonyesha kitchen party?

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha....Mkuu hii ni kali,umenifungua macho sana,kumbe watanzania bado sana kwenye tasnia ya habari.
 
Hivi kituo gani cha redio Kenta na mtangazajii wake walipelekwa ICC the Hague na Ocampo?

Sijui kama hao TBC1 History kwao have anything to go by. Uchochezi wao ni MAUTI kwetu tena mbaya zaidi wanaufanya kwa KODI zetu. Mara ya mwisho nilivyo check profile ya TBC1 nimeona ni Taasisi ya Serikali na mshahara wa huyo mtangazaji tunamlipa sisi through kodi zetu (READ SIO KODI ZA CCM) Correct me if I'm wrong.
 
achana nayo hiyo tbc1,kazi kubwa umbeya tu.lini utakuta cnn au bbc wanaonyesha kitchen party?
Nashukuru kwa kuufanya moyo wangu ujae furaha ya kebehi kwa kituo hiki kuonesha hadi kitchen party.
 
achana nayo hiyo tbc1,kazi kubwa umbeya tu.lini utakuta cnn au bbc wanaonyesha kitchen party?
Hallow i salute you!ckutaka kununua vocha,nikajua ntaangalia tbc tu,kwa hasira ulizonipa bora nikanunue vocha tu
 
Hivi watu wenye akili timamu bado wana angalia mavi yanafanywa t.b.c dhidi ya chadema?hii sio television ya taifa taifa
 
Wamebakia kushabikia CCM wanashindwa kujiendesha kabisa hata hapo studio ukienda au chumba chao cha mapumziko ni taka taka tuu hata CLOUDS wamewashinda kwa mbali hawana kamera za kutosha Station ya Taifa ya hovyo kabisa ,kabisa hata wakati wa mwalimu akina Ben Kiko walikuwa na uwezo wa kutetea maslahi ya nchi si hawa wa leo makanjanja
 
Hivi watu wenye akili timamu bado wana angalia mavi yanafanywa t.b.c dhidi ya chadema?hii sio television ya taifa taifa
Kuna Maeneo mengine inaonekana TBC tuu kwa hiyo wana influence
 
......Leo kwenye kipindi chao kinachorushwa kuanzia saa saba mchana kinachoitwa Dira ya mchana,TBC1 wametangaza habari ambayo naweza sema kuwa ni propaganda chafu zinazotumiwa na CCM kudhoofisha nguvu ya vyama vya upinzania hasa CHADEMA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kule Arumeru Mashariki.

......Akiripoti mwandishi wao amedai kuwa kuna wanachama wa CHADEMA na TLP wamejiunga CCM akiwepo M/kiti wa jumuiya ya wazazi wa TLP..cha kushangaza huyu mwandishi ameonyesha kadi ameonyesha kadi zisizopungua 10 za TLP na KUSHINDWA KABISA KUTUONYESHA KADI ZA WANACHAMA WA CHADEMA..Hii naweza sema ni mchezo mchafu na wakitoto tena unaorushwa na kituo chenye dhamana ya kulinda maslahi ya UMMA bila kulalia upande mmoja...napata taabu kufikiri kuwa mbona huyu mwandishi akutoonyesha kadi za CHADEMA? na mtu atahitwaje mwanachama wa CHADEMA bila kuwa na kadi?

......Ombi langu kwa chumba cha habari TBC1 wanapaswa kujua kuwa habari zao tunazisoma na kuzisikiliza na kuziona..utumbo wanaofanya kuna siku utawagharimu..na niwakati wa hawa waandishi wa hiki kituo cha habari kuzingatia weledi badala ya kuendelea kulalia CCM utadhani kuwa CCM watatawala milele.

TBC1 kumbukeni kilichowakuta KBC KANU ilivyoondoshwa madarakani, hakiko mbali sana nayi mpaka mfagiaji nji swaga moja tuuu.. shenzikabisa
 
hawa tbc watakuwa na tatizo, yawezekana ni ugonjwa wa tibii..
 
Achana nao vyombo vya habari vilishikiliwa na GHADAFI kule Libya sasa yuko wapi?
 
waandishi wengi wa TBCI hupenda kufurahisha viongozi ili wapangiwe tripu nao wale posho! hawana inshu wala habari waendelee na hizo kitchen party zao.
 
Back
Top Bottom