TBC mbona mnahoji upande mmoja ?

TBC mbona mnahoji upande mmoja ?

swagazetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
4,253
Reaction score
1,475
Mimi jana nilikuwa dar maeneo ya posta na baadae IFM nilibahatika kuhojiwa na mwandishi wa TBC( )kuhusu mapokeo ya hotuba ya rais kikwete na rafiki yangu pia akahojiwa vilevile lakini cha kushangaza mawazo ya wachambuzi makini hayatangazwi TBC kama maoni ya watanzania wanaleta mawazo ya wale wanaoisifia tu kwa bahati mbaya kazi yangu hainiruhusu kuwa wazi lakini kimsingi Tbc wapo kwenye kampeni na ukiangalia hotuba hii haikubaliki kwa wengi sana.

Tbc hawaoni aibu.ili habari ivutie lazima iwe na changamoto sasa tbc wao kila aliyehojiwa kapongeza!!! Kila aliyeulizwa kampongeza rais kivipi?k hajui kubalance habari jifunzeni Check in balance ya habari.

Tbc mnakera sana.kikwete anekuwa miungu mpaka kila mtu amsifu? Ampongeze?
 
Waswahili wanasema ukiona mtu anapenda kusifiwa ujue..............? Jibu utalipata kupitia slogan ya Mnyika.
 
Mimi jana nilikuwa dar maeneo ya posta na baadae IFM nilibahatika kuhojiwa na mwandishi wa TBC( )kuhusu mapokeo ya hotuba ya rais kikwete na rafiki yangu pia akahojiwa vilevile lakini cha kushangaza mawazo ya wachambuzi makini hayatangazwi TBC kama maoni ya watanzania wanaleta mawazo ya wale wanaoisifia tu kwa bahati mbaya kazi yangu hainiruhusu kuwa wazi lakini kimsingi Tbc wapo kwenye kampeni na ukiangalia hotuba hii haikubaliki kwa wengi sana.

Tbc hawaoni aibu.ili habari ivutie lazima iwe na changamoto sasa tbc wao kila aliyehojiwa kapongeza!!! Kila aliyeulizwa kampongeza rais kivipi?k hajui kubalance habari jifunzeni Check in balance ya habari.

Tbc mnakera sana.kikwete anekuwa miungu mpaka kila mtu amsifu? Ampongeze?

Ndugu, unashangaa nini. TBC NI TV YA CCM na wala Si ya Taifa. Kama haufahamu muulize Mzee........ aliyekuwa mkurugenzi wa TCB aliyeondolewa kwa fitina za mtu aliyemuondoa kwenye vyombo vya kimataifa!.

Dawa ya Mhe Raisi tushirikiane katika kutoa elimu kwa watanganyika na hasa wa vijiji ili katiba "mbaya" inayotarajiwa kuletwa kwetu tukatae.
 
Kilichopo sasa hivi ni mkakati wa CCM na serikali yake kuhonga vyombo vya habari!,, Kwa kifupi serikali iko hoi inachofanya ni kuhakikisha habari mbaya dhidi yao hazitoki... Vyombo vya habari makini vimebaki kama sio Kimoja viwili
 
Tbc Tangu Aondoke Tido Mhando Sikuwahi Kurudi Tena Kuitazama

Bahati mbaya kabisa kabisa wengine hatuna jinsi ya kuikimbia pale unapotaka kufuatilia jambo fulani muhimu..ila naamini siku zote kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na incha
 
Nyie mnaoponda Television yetu ya Taifa ni mazuzu.

Nawauliza mmejuaje kuwa huwa inahoji upande mmoja kama huwa hamwangalii?

Haya endeleeni kuangalia tv zingine na filamu zenu za kifilipino ili muwe wazungu.
Lakini sisi Watanzania wa bara na visiwani, mijini na vijijini tunaangalia TBC1.

Ukweli na uhakika.

Kama ukiponda tu, wewe nakuhesabu kuwa ni mtazamaji mwaminifu, maana huwezi kumtukana mtu usiyemjua.

Endeleeni kuhabarika na habari za Taifa na Kimataifa kupitia Tanzania Broadcasting Cooperation.
 
Huwa natamani kungekuwepo na button ya dislike sababu ya post kenge kama hii
 
TBC ni TV ya wanzalendo nyie mna ile tv yenu nyingine?
 
Tatizo lako ni kuwa unadhani mnavyochangia hapa ni sawa na mitaani. Watu wameikubali hotuba sasa wewe unakuja na yap yap na nn?
 
Tbc ni ya ngekise sana

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom