TBC-1: ya nini yote haya???

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
TBC-1 leo wametudhihirishiwa wazi kuwa wanafanya kazi kwa maagizo maalumu ya Serikali. Kuna habari toka Dodoma walikuwa wanairusha katika taarifa ya habari ya usiku huu wa saa mbili. Mhe. Waziri Mkuu wakiongea na viongozi wa madhebu ya Dini kuhusu masuala mbalimbali hasa la mustakabali wa Katiba..habari hii ambayo iliandaliwa na Victoria Patrick wa TBC Dodoma, ilionyesha wazi kuwa imegoma kwenda hewani, ilikwaruza n.... . Lakini cha kushangaza, wasoma habari wa TBC akiwemo JOYCE KINGALAME waliing'ang'ania zaidi ya mara tatu kuitoa hewani lakini bila mafanikio wakasema "Victoria Patrick hayupo tayari..tuendelee na habari nyingine .

Cha kusitaajabisha, mwisho kabisa mwa hitimisho la habari kabla ya kuingia habari za michezo, wakairejea tena hiyo habari ya Dodoma wakisema ...habari yetu ya Pili....sasa mwandishi wetu Victoria Patrick yupo tayari toka Dodoma.....

Tofauti na habari nyingine ambazo zikigoma wanazipotezea, lakini hii ya leo ni ya kustaajabisha kwa TBC.
 
they always being manipulated................SISHANGAI.
 
Hao hawana maana kabisa ndio maana walimtoa Tido ili wafanyw upuuzi wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…