TBA wapewe jukumu hili Dodoma

ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Posts
1,885
Reaction score
4,014
Wazalendo na wataalamu wa TBA ni kielelezo cha ubora wa mainjinia wetu wa ndani na uzalendo mkubwa walio nao
Vibaraka wa mafisadi na mabeberu wali zoom picha wanazodai ni nyufa za Jpm hostels ili kuharibu jina la wazalendo hawa wa TBA
Wazalendo hawa wamejenga zile hostel kwa gharama ya billion 10 tu na ndo maana wapiga deal wamekasirika maana wao walitaka bilion 90
Wote tumesikia utaalamu waliotumia TBA kujenga hostel zile,ni technic kali yaani HOSTEL ZINAPUMUA,expansion joints
Ni wakati sahihi na uamuzi wa kizalendo majengo yote mapya ya mji mkuu wa dodoma yajengwe na TBA kwa future nzuri ya nchi yetu na gharama ndogo,tena yatapendeza majengo yote mapya yawe yanapumua kwa pamoja
 
tehh.teehhh...teehhhh.....[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Mbona ndio wanaoijenga Dodoma kwa sasa? Majengo yote ya serikali wao ndio wakandarasi
 
Kuna liprofrofesa la UNISA kila mara linasema Elimu yetu ya degree Bongo sawa na certificate sehemu zingine kila kauli zinatolewa na wasomi hovyo likipata linanitumia...linasema hao ndio Picha ya wasomi wenu...
 
Yakipumua inapendeza! Kwa bahati mbaya kulikuwa na kosa la kiufundi likasababisha jengo moja tu kupumua! Lengo lilikuwa yapumue kwa pamoja!
Lakini tusivunjike moyo, tuendelee kusubiri na mengine yote yapumue! Yaliyobaki yakipumua kwa pamoja itapendeza!
Upumuaji Mpya wa kisasa wa majengo umegunduliwa bongo, zig zag! Itabidi wazungu waje tuwape hii teknologia Mpya kupumulisha majengo kwa zig zag! Inapendeza!
 
Achana nao hao TBA
wameshashindwa kujenga na wanaelekea Chato kujenga Hospital ya Rufaa huko
ni bora hata mifuko ya kijamii imeweza na ingewapatia nyumba za malazi bora wageni wote
lakini kwa sasa hata Watumishi wa Serikali wamepewa Notisi na TBA waondoke nyumba zilizokuwa za Serikali, za Manispaa na hata Msajili wa Majumba ili kupisha ujio wa Wafanyakazi wapya kutoka Dar es salaam
TBA bado kabisa
kuna maghoroga ya UDSM yaliyojengwa na muIsrael mpaka leo hayana nyufa, sembuse hayo yaliyokaliwa wiki 4
 
Huu utaalam mpya kabisa wa kupumua zig zag uandikiwe paper kwenye International Journals! Hii Teknologia tuiuze tupate pesa ndefu zitakazotusaidia kuelekea kwenye uchumi wa kati! Mimi nimeipenda! Tatizo tulikuwa hatuijui hivyo imetutia hofu! Lakini wataalam wetu wametuambia tusiwe na hofu! Bongo hii!!!
 
Miezi 8 sio mchezo upumuaji hule utaletea shida tu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…