TAZARA ya SGR itakuwa " white elephant" lingine kupitia TOZO

TAZARA ya SGR itakuwa " white elephant" lingine kupitia TOZO

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,435
Reaction score
1,995
Asalam aleikhoom wana JF!

Baada ya kusikia kwamba kuna mpango wa kuanzisha project kubwa ya SGR TAZARA kabla ya project aina hiyohiyo ya TRC kukamilika binafsi nilistuka sana! Hadi sasa najiuliza hivi nchi hii imelogwa na nani?

Kwasababu sikutegemea kabisa kwamba kabla ya kukamilika kwa SGR ya TRC na mradi mkubwa wa hydropower Kihansi na mingine kama bomba la mafuta la Hoima-Tanga, kwamba Tanzania ingeanzisha au hata kufikiria kubuni tena mradi mwingine usiojulikana faida yake katika mazingira ya kiuchumi sasa na siku zijazo!

Tatizo la TAZARA ni kukosa mzigo upande wa Zambia bas! Na hii ni kwasababu Zambia wana mashirika mawili ya reli: TAZARA na Zambia railways halafu reli zake ni Cape gauge.

Mzigo wa Zambia kupitia TAZARA kuja Dar es Salaam ulipungua sana baada ya utawala wa makaburu South Africa kuondoa. Lakini hata kabla ya "uhuru" wa SA sehemu ya mzigo wa Zambia umekuwa unapita Msumbiji mpaka bandari ya Beira au Maputo.

Zipo sababu nyingi na za msingi za Zambia kupitisha mzigo wake SA au Mozambique lakini nani asiyejua matatizo ya TAZARA baada ya kukosa mzigo wa Zambia? Hata mzigo wa upande wa Tanzania nako ni matatizo kutokana na ushindani wa usafiri wa barabara.

Lazima tukubaliane kwamba katika mazingira ya sasa reli haiwezi kushindana na barabara nzuri za lami.

Na hilo ndiyo litakuwa tatizo kubwa la SGR ya TRC ambayo inajengwa sambamba na meter gauge ya mkoloni ambayo lishanyan'ganywa mzigo kwa ushindani wa usafiri wa barabara!

Kwahiyo kama hali ndiyo hiyo mzigo wa SGR mpya ya TAZARA utatoka wapi?

Kwahiyo mpaka sasa hatujaona kwamba tunapigwa au tunajipiga wenyewe vita ya kiuchumi kwa kujipa jukumu la kugharamia miradi kama hii kwa kutegemea uchumi wa majirani zetu.

Tulisapoti vita vya ukombozi kusini SA, Zambia, Zimbabwe, Mozambique na Uganda kwa gharama kubwa za uchumi wetu. Matokeo yake nchi hizo baadhi wametupita kiuchumi na hawana habari na sisi!

Kenya wanayo SGR kati ya Mombasa na Nairobi; lakini inasemekana tayari iko hoi kutokana na ushindani wa usafiri wa barabara. Nenda China, USA, Europe au kokote kwenye network nzuri ya highways, biashara ya reli HAINA FAIDA. Tutaogezewa tozo tu!

Last but not least! Kutokana na vita ya Russia na Ukraine uchumi wa dunia uko hatarini na nchi kama Tz tayari bei ya mafuta inapanda kila mwezi! Badala ya kubuni white elephant lingine tupunguze mateso zaidi kwa Mtanzania.
 
Usafiri wa reli ni rahisi na nafuu sana kuliko wa barabara, tatizo letu ni uongozi kushindwa kuelewa namna ya kusimamia.

Kukosekana mzigo kunatokana na viongozi wa nchi kuwekeza kwenye uchukuzi wa barabara, hawa viongozi wanapata faida kubwa sana huku wakituachia mashimo kwenye barabara ambazo wao ndio wanaotafuta tenda za ujenzi. Tazara imara inaweza kubeba mizigo si ya Zambia pekee bali ya Kongo, Zimbabwe na Malawi.

Mwisho ujenzi wa reli hiyo si wa Tanzania pekee bali Zambia pia inahusika kwenye gharama.
 
Kila siku huwa nasema sijawahi muelewa yule alikuwa anaitwa Baba wa Taifa..

Yaani kutumia rasilimali za Taifa kusaidia Nchi zingine bure kabisaa bila hata kuwakopesha,aisee this is shit..

Pili nadhani sgr ya Tazara itaanza kujengwa baada ya sgr tembo mweupe ya Mwanza kukamilika may be 2027 huko..

Kuhusu mzigo sina shaka na hilo kwa sababu ikiwa sgr speed itakuwa kubwa kuliko malori,na usafiri wa barabara ni WA ku compliment reli sio kushindana na reli maana reli haiwezi kufanya Kazi za distribution ya mzigo..

Mwisho tujuze Uchumi wetu Ili mizigo ya Nchi jirani iwe ina substitute au kujalizia mizigo yetu sio tunajenga kwa ajili ya eti Zambia au DRC au Malawi nk..So kabla ya kufikia uamzi huo lazima tuwe tumefikia kiwango fulani cha GDP Ndio tujenge..

Hiki kilichofanyika cha kujenga sgr pambo kwa sababu za kisiasa huku tukioumia ni upuuzi na usirudiwe.👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220802-205101.png
    Screenshot_20220802-205101.png
    114.5 KB · Views: 31
  • Screenshot_20220802-205049.png
    Screenshot_20220802-205049.png
    117.7 KB · Views: 26
Watu wengine wanaboa mpaka Sasa hivi mtu na mindevu yake hajui faida ya reli ukilinganisha na Barbara ww kauze Hilo lorry lako tuu isituaribie barabara
 
Back
Top Bottom