KERO TAWA na TFS kinachokwamisha mchakato wa ajira zake ni nini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hizi ajira zao zilitangazwa mnamo mwaka jana mwezi wa nane (Agosti 2024) mpaka kufikia leo mchakato wake haujakamilika.

Tukiangalia taasisi kama Tanapa, Uhamiaji, Polisi pamoja na Magereza mchakato wao huwa unakamilika ndani ya miezi mitatu au miwili

Je, kinachokamisha hizi taasisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania(Tanzania Wildlife Management Authority - TAWA) zishindwe kuajiri kwa muda muafaka ni kitu gani mpaka sasa ni miezi 7 hakuna kitu kinachoelewaka.

1. Je, ni uzembe wa baadhi ya watu.?
2. Je, bajeti hakuna na kwa nini watangaze ajira ?

Wadau tushirikiane kutoa maoni juu ya hili...
Vijana mtaani waliosomea taaluma ya uhifadhi wanateseka sana, maana mtu anakaa miezi karibu saba au nane mchakato bado unataka uende mpaka mwa mzima.

My country 😭 😭

Learn or perish
 
KUBWA KWA WALIOITWA KWENDA KOZI TAWA – TUNAIOMBA SERIKALI ITUSAIDIE!
Ni jambo la kushangaza na kusikitisha kuona jinsi wenzetu waliopata nafasi kwenye taasisi kama TFS, TANAPA, JWTZ, JKT, POLISI, na Magereza mfano ni taasisi ya TFS wameshaondoka mtaani shida inakuwa nini kwa hawa wa tawa...
Pia
wanavyopokelewa kwa heshima, wanapewa taarifa mapema, na kusaidiwa kwa hali na mali katika maandalizi ya kozi zao.
Lakini hali ni tofauti kabisa kwetu tuliopata nafasi kwenye Taasisi ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA). Vijana wetu wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi zikiwemo:
  • Kukosa msaada au mwongozo kutoka kwa mamlaka husika.
Hii inaleta hisia kwamba TAWA inadharauliwa au haitiliwi maanani kama taasisi nyingine, jambo ambalo linakatisha tamaa vijana walioteuliwa na waliokuwa na ndoto za kulitumikia taifa katika sekta ya uhifadhi wa wanyamapori.
Tunaiomba TAKUKURU, Tume ya Utumishi wa Umma (PSRS), na vyombo vingine vya serikali:
  • Kufuatilia kwa ukaribu mchakato wa upangaji na maandalizi ya kozi hizi,
  • Kuhakikisha kuna usawa na haki kama ilivyo kwa taasisi nyingine za serikali,
  • Na kama kuna uzembe, upendeleo au upotoshaji – wachukuliwe hatua stahiki.
Kama wazazi wa vijana wa Kitanzania, hatuombi kupendelewa, tunachoomba ni haki, usawa, na mazingira rafiki ya kutimiza wajibu wetu kwa taifa.
Tunaamini serikali yetu kupitia wizara husika italisikia hili na kuchukua hatua haraka.
#TAWA #ChangamotoKozi #TunaombaMsaada #TAKUKURU #Utumishi #HakiKwaWote
 
Kama umeshaitwa kazi subiria tu utaitwa kwenda mafunzo ya kijeshi, Anza mazoezi
 
Vipi Vijana Mlioenda Mlele Msharudi ama Bado?

Na hiizi Nafasi Mpya wanaenda lini, Maana ni mwezi sasa Ushakata
 
Back
Top Bottom