Tatizo sio ccm... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo sio ccm...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kijakazi, Jul 23, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  TATIZO SIO CCM NA WALA SULUHISHO SIO CHADEMA!

  Ninachomaanisha hapa ni kwamba matatizo kwenye jamii yetu kama umaskini na kadhalika yapo sio kwa sababu tu eti CCM iko madarakani, la hasha!

  Mimi naamini chimbuko kubwa la matatizo yetu ni utamaduni wetu, jinsi tunavyolelewa kwa hiyo hata kama leo CCM wataondoka na wakaja CHADEMA au CUF hakuna kitakachobalika na miaka kumi baadae tutakuwa bado tunalalamika tu!

  Labda niulize hivi ni nini kinatufanya tuamini kwamba wapinzani watafanya tofauti na CCM sasa hivi? Hawa wapinzani wanatokea Sayari nyingine? nikiimanisha wamekulia na kulelewa Sayari nyingine? kama jibu lake ni HAPANA basi hata mabadilko kutoka kwao pia kutakuwa HAKUNA!

  Nitaelezea kwanini, kwanza mimi naamini maendeleo yanatokana na utamaduni wa jamii husika, kwa hiyo basi kama jamii husika haina utamaduni ambao unalea na kukuza watoto wao wawe raia wema na waliostaaribika hakuna miujiza itakayotokea kuwafanya waendelee.
  Kwa hiyo basi kwa mfano nikimuangalia Raisi Kikwete sioni tofauti ya tabia zake na mtanzania mwingine yeyote wa kawaida aliyelelewa TZ, kuanzia baba zetu, kaka zetu, wajomba zetu n.k
  Kwa mfano watz wengi wanalalamikia Ubinafsi wa viongozi wetu, bila kuelewa kwamba ubinafsi umejikita ndani kabisa ya utamaduni wetu, kwa mfano asilimia kubwa ya baba zetu nyumbani hawajui watoto wanakula nini, ananunua maharage kila siku nyumbani lkn yeye anakula nyama choma nje na katu hali hayo maharage sasa kuna tofauti gani na Kikwete au Pinda au Zito anaekwenda kutibiwa nje na sio kwenye Hospitali ambazo yeye ndio mwenye jukumu la kuziboresha?

  Ni mara ngapi unakwenda kwenye sherehe unakuta kuna watoto wadogo kabisa na ikifika saa ya kula wakubwa ndio tena mizee na mi mama yenye vitambi inakimbilia kupanga mstari ili ile kwanza kwa nini wasiwape watoto wadogo kwanza? Je kuna tofauti gani na akina Kikwete?

  Ingawaje unaweza ukaona ni vitu vidogo sana lakini ukumbuke viongozi wetu ndio wanatokea humu humu na wamelelewa ktk hayo mazingira hivyo mimi nasema hata kije Chama gani labda kisiongozwe na watu waliolelewa na kukuzwa na huu Utamaduni wetu!

  HAYO NI MAONI YANGU!

   
Loading...