MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 15,891
- 40,167
Well, chupa iwe ya 200ml na tukiamua kuuziana kwa tots?wameshaeleza na wamesema chupa zinazotengenezwa ziwe kuanzia 200ml
SA TUNAHAMIA KWENYE BALIMIHabari za mchana wana JF
Nimebahatika kufanya tafakari kidogo kwenye hili swala la viroba, kinacho nitatiza ni kujua je tatizo ni viroba au wanywa viroba?
Tofauti na madawa ya kulevya ambayo yenyewe peke yake ni haramu kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini kiroba kama kifungashio au kinywaji kilichopo ndani yake si vitu ambavyo ni haramu kwa minajili ya sheria zetu.
zipo tafsiri ambazo siyo sahii kwamba pengine vifungashio vinaweza vikawa vinachafua mazingira na mawazo mgando ya namna hiyo. Ila bado suluhisho makini halijapatikana. Upo uwezakano wafanyabiashara hawa wanaouza hizo pombe wakaja kwa namna nyingine, wakaweka ujazo mdogo wa pombe hiyo hiyo kwa style nyingine. Sasa lazima serikali ileleze bayana inachozuia ni vile vikaratasi vinavyofungia pombe, pombe yenyewe au pombe yenyewe kwenye ujazo mdogo.
Nawaza kwa maandishi tu, Aksanteni
umemaanisha kumimina kuuza kwa viglass ka vile vya gongo?Well, chupa iwe ya 200ml na tukiamua kuuziana kwa tots?
Yah!umemaanisha kumimina kuuza kwa viglass ka vile vya gongo?
itakua ubunifu wa hali ya juu
dah hii idea ya biashara ni yakufanyia kaziYah!
Umeeleza mambo yanayotaka kufanana na point, lakini lazima ujue kwamba hoja kwamba kifungashio cha kiroba hakiozi haina mantiki, kuna material nyingi sana haziozi kama vile chuma na aluminium lakini vinafanyiwa recycling hivyo basi suala siyo material, swala ni kutokuwa na technology ya kushughulika na taka ngumu. Ukiachilia hilo, hoja yako nzima imelenga kwenye udhaifu wa kuwadhiti wanywaji. Udhaifu wa kudhibiti watoto wasinywe viroba na madereva au watu wengine. Hivyo basi udhaifu huo usiwe chanzo cha kunyima raha wanywaji wengine wanaofuata utaratibu. Kama wazalishaji na watumiaji wakijiunga pamoja wakaishitaki serikali, wanazo hoja za msingi.Kama hujaelewa ubaya wa viroba upo katika sehemu tano. Kwanza vinauzwa kwa bei ndogo sana hivyo watoto wadogo wa shule wanaweza kutumia pocket money yao ndogo wakavinunua. Watoto wadogo wengi sana wameshageuka walevi. Pili kiroba kwa udogo wake kinaingia mfukoni kirahisi. Aliyekibeba hajulikani. Akiwa dereva wa basi anaweza akabeba vingi mfukoni. Mbele ya safari akivinywa akilewa anaangusha basi. Wewe unayevitetea ukavunjika kiuno au kufa kabisa. Tatu kifungashio cha kiroba hakiozi kwa hiyo ni uharibufu mkubwa wa mazingira. Mbuzi au ng'ombe akitafuna kiroba kitupu kwenye majani anakufa. Nne: Wajanja wachache wanafunga gongo ndani ya vifungashio vya kiroba na wanywaji wanafikiri ni pombe halali kumbe ina sumu kali na inaharibu miili ya hao wanywaji. Kwa sababu ya udogo wake viroba vinaweza kufichwa kirahisi mahali popote na kuuzwa kwenye maduka ya kawaida. Kwa hiyo mtoto anatumwa unga dukani ndani anawekewa kiroba. Akitoka hapo anatoa kiroba chake anapeleka unga nyumbani. Akitoka kwenda kucheza ndipo anakunywa hiyo pombe
Sasa hayo maelezo wanayatoa wakati wawekezaji wamekwisha ingiza pesa zao kununulia raw materials na viroba vimekwisha tengenezwa viko kwenye mzunguko, hiyo hasara nani atakaye wafidia, ni Tanzania tu ambapo watu wanafikiria kuanzia mbele kwenda nyuma.wameshaeleza na wamesema chupa zinazotengenezwa ziwe kuanzia 200ml
Ikamulie hukohuko kiwandani!Kwa hiyo nikikamulia kwa chupa ya maji ya kilimanjaro hamna faini siyo? Hahahaahahhaah
Hongera sana serekali yangu, tukimaliza hili turudi kwenye mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali.
Nafikiri tena kwa maandishi, kilichopelekea viroba vizuiwe ni unywaji hatarishi wa hiyo pombe sasa basi ikiwa vifungashio vitaongezwa ujazo, je hiyo ndiyo njia ya kitaalamu ya kupunguza au kuzuia unywaji hatarishi? Mimi nahisi kuna matatizo katika namnya yetu ya kufikiri na kusuluhisha matatizo, labda tatizo lenyewe hatujalijua hivyo utatuaji wake unakua mgumu zaidi.Tatizo ni vifungashio aina ya viroba!
tunahitaji pombe yenye radha ile ile ije na muonekano wa chupa zaidi ya mil200
Hii itapunguza tena kwa kiasi kikubwaNafikiri tena kwa maandishi, kilichopelekea viroba vizuiwe ni unywaji hatarishi wa hiyo pombe sasa basi ikiwa vifungashio vitaongezwa ujazo, je hiyo ndiyo njia ya kitaalamu ya kupunguza unywaji hatarishi. Mimi nahisi kuna matatizo katika namnya yetu ya kufikiri na kusuluhisha matatizo, labda tatizo lenyewe hatujalijua hivyo utatuaji wake unakua mgumu zaidi.
Watengeneza viroba wanawajua wateja wao unafikiri atawatawaletea kitu kitakachokuwa ndani ya uwezo wa wanywaji wao?Hii itapunguza tena kwa kiasi kikubwa
Kiroba kinanunulika kwa bei rahisi tofauti na ujazo utakaoobgezwa tena kwa kifungashio cha chupa
Pia urahisi wa kutembea na kubeba chupa ni tofauti na kiroba