Tatizo ni mwanaume au mwanamke?

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,585
1,885
Waungwana,

Mbona hili swala la watu kulalamika juu ya haya mapenzi kuwatesa tatizo ni la nani hasa? Maana wanawake wanalalamikia wanaume na wanaume wanawalalamikia wanawake, hivi nani chanzo cha matatizo kwenye mahusiano tukianza kupembua kuanzia hulka za ndani kabisa nani chanzo kati ya mwanaume na mwanamke?
 
chanzo ni aliyeanza kuumbwa ndio mwenye matatizo na uthibitisho wa hili kuwa wanaume ndio tuna matatizo upo kwenye biblia maana imisha eleza kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu na tuishi nao kwa akili.ukiona mwanamke ana enda ndivyo sivyo basi jua fika mwanaume ndio mwenye tatizo,kama alivyoumbwa toka ubavuni mwako una uwezo wa kum shape utakavyo ww
 
Tatizo ni nyakati tu....
Siku hizi watu wanatongozana 24/7
mkeo yupo facebook,instagram,twitter,JF,watsaap....kutwa anabandika picha za kuonesha
anavyopendeza na alivyo umbika
na wewe kutwa uko huko unatongoza wengine
ndoa ikidumu hata mwaka shukuruu mungu
 
SIMU ndo yakulaumiwa,,,,,, anaebisha tuamue kuanzia LEO simu zisifanye kazi na watu wasiishi na simu alafu TUONE matokeo yake. mtu yupo TZ ila anawasiliana na michepko ya korea/ urusi huku ndani mke / mme akikutext tu jibu unapata jion tena kwa mdomo.
 
Tatizo ni nyakati tu....
Siku hizi watu wanatongozana 24/7
mkeo yupo facebook,instagram,twitter,JF,watsaap....kutwa anabandika picha za kuonesha
anavyopendeza na alivyo umbika
na wewe kutwa uko huko unatongoza wengine
ndoa ikidumu hata mwaka shukuruu mungu
Kweli kabisa ukitimiza mwaka basi toa Sadaka kumshukuru muumba wako...
 
Back
Top Bottom