Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 16,669
- 21,874
Ukiangalia Afrika nzima kwa makini utagundua kuwa Tanzania ni nchi pekee ambayo ina raslimali nyingi kulliko nchi nyingie yoyote. Kuna madini, gesi, mafuta ardhi yenye rutuba na vivutio vingi vya asili. Lakini ukiangalia tena kwa haraka haraka utagundua pia kuwa Tanzania ni nchi inayojikongoja sana kimaendeleo kuliko nchi nyingi za Afrika. Hapo ndipo swali la thread hoii linapokija, je tatizo liko wapi?
Jibu ni fupi sana; winaonekana kama vile watanzania tunatawaliwa na sifa mbili kubwa.
(1) Tunapenda sana njia za mkato. Jirani akifanya jambo akafanikiwa basi na mimi nifanye vivyo hivyo. Hili sina haja ya kufafanua zaidi ila liko wazi kabisa. Watanzania wengi hatuna ubunifu; na hata wale wenye wanaojaribu kuwa wabunifu, huishia kukopi kwe wengine, hasa kwa kutumia kolabo, na kujifanya wamebuni. Utashangaa kuwa hata serikali yetu hufanya vivyo hivyo, yaani kuiga toka nchi za jirani.
(2) Ni wepesi wa kuridhika. Wengi wetu tukifanya jambo likatunyanua kidogo tu, basi tunaridhika mapema sana na kuishia hapo hapo ambayo ni stage 2. Nadhani hili ndilo tatizo kubwa sana kwetu; hatujua kuangalia stage 3, stage 4 na nyinginezo zina nini..
Tufanyeje? Inabidi twende nje ya hapo.
Leo nimeandika baada ya kuangalia video nyingi za muziki wa kutoka Tanzania na video mbalimbali za hotuba za viongozi wetu. Inawezekana hayo niliyooana hayareflect tabia za watanzania kikamilifu, ila kwa jinsi ninavyowajua watanzania wenzagu ni wazi kuwa hata kukiwa na tofauti zitakuwa ni ndogo sana