Tatizo letu hatuna vipaumbele. Viongozi onyesheni Uongozi.

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
1,314
Baba wa Taifa Mwl Nyerere alisema maadui wa Taifa hili ni watatu (UMASKINI, UJINGA & MARADHI). Viongozi wetu hasa vijana wangejielekeza kupigana vita na maadui hawa badala ya kufanya porojo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza alipofika aliwatahadharisha "machangu" na kusema kiama chao kimefika. Mkuu wa mkoa wa Dar anaendelea na mradi wake mkubwa wa kupiga vita ushoga, uvutaji wa sigara na shishe. Lakini jambo la kujiuliza "Hivi ndivyo vipaumbele vyetu?"

Nilisoma ripoti ya uchumi ya Mwaka 2012 kuhusu uchumi wa ulaya na Afrika. Katika ripoti hiyo Ubelgiji ilionekana kuwa na uchumi mkubwa zaidi ya nchi zote kwa ujumla wake zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara (ukitoa Afrika Kusini).

Hebu viongozi wetu onyesheni "UONGOZI" kwa kujielekeza kwenye vipaumbele vitakavyokuja kuinua maisha yetu.
 
Back
Top Bottom