Tatizo la Zanzibar sio muungano

Tatizo la Zanzibar sio muungano

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Wako Wazanzibar ambao wanadhani hali yao ya maisha itaboreka kama wakijitenga kutoka bara, mimi sidhani kama itakuwa hivyo. Tangu 1964 ya Muungano, Zanzibar ilipewa fursa ya kipekee ndani ya muungano ya kujiamulia mambo yake mengi yenyewe bila ya kuingiliwa na serikali kuu wala watu wa Tanganyika.

Wazanzibar sio wengi ukilinganisha na wakazi wa Wilaya za Bara sebuse mikoa.

Kutokana na hali ya kijografia ya Zanzibar ningetarajia Zanzibar ingekuwa kitovu cha uvuvi, usafiri majini na bandari kubwa nchini na Africa Mashariki lakini hili halikutokea na wala halitokei. Ukiwauliza wanasingizia Muungano.

Wako busy na Zanzibar ni nchi, Zanzibar ni nchi kila siku na siku zote. Wazanzibar hawataki nchi bali wanachotaka wao ni maisha mazuri kiuchumi, na hii ndiyo inayosababisha wazanzibar wengi wametawanyikia Tanganyika, Dubai, UK, Emirates, n.k kutafuta uchumi.

Viongozi wa Zanzibar badala ya kununua meli kubwa za uvuvi na usafiri na usafirishaji wanatumia hela nyingi kugharamia Ikulu, Mikoa mingi(vijimikoa), Wilaya nyingi(vijiwilaya), Tarafa, Kata na vijiji.

Zanzibar inagharamia bunge na baraza la wawakilishi. Zanzibar ilitakiwa kujiendesha kama jimbo/mkoa maalum ndani ya Tanzania kwa kivuli cha Muungano na sio nchi ili kupunguza gharama zake za uendeshaji kama vimulimuli, mabenzi, kutunza wastaafu, mishahara ya Rais na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na watumishi wengine ndani ya kivuli cha "Zanzibar ni Nchi".

Hata kama Zanzibar itajitenga, hali ya maisha ya wananchi wake haitaboreka kama inavyodhaniwa, badala yake Zanzibar itakuwa lango kuu la uhalifu kama vile biashara ya madawa ya kulevya, ushoga, na ugaidi.

Kwasababu sioni kitu chochote kinachosababishwa na Muungano kinachoifanya Zanzibar isiwe na meli na viwanda vya mazao ya uvuvi, isiwe na meli za usafiri na usafirishaji, isiwe mzalishaji mkuu wa karafuu na mbata duniani.

Badala yake Bakhessa ndiye mwenye meli za uhakika zinazotoka na kuingia Zanzibar.
Zanzibar Oyeee!!
 
Wako Wazanzibar ambao wanadhani hali yao ya maisha itaboreka kama wakijitenga kutoka bara, mimi sidhani kama itakuwa hivyo. Tangu 1964 ya Muungano, Zanzibar ilipewa fursa ya kipekee ndani ya muungano ya kujiamulia mambo yake mengi yenyewe bila ya kuingiliwa na serikali kuu wala watu wa Tanganyika. Wazanzibar sio wengi ukilinganisha na wakazi wa Wilaya za Bara sebuse mikoa. Kutokana na hali ya kijografia ya Zanzibar ningetarajia Zanzibar ingekuwa kitovu cha uvuvi, usafiri majini na bandari kubwa nchini na Africa Mashariki lakini hili halikutokea na wala halitokei. Ukiwauliza wanasingizia Muungano. Wako busy na Zanzibar ni nchi, Zanzibar ni nchi kila siku na siku zote. Wazanzibar hawataki nchi bali wanachotaka wao ni maisha mazuri kiuchumi, na hii ndiyo inayosababisha wazanzibar wengi wametawanyikia Tanganyika, Dubai, UK, Emirates, n.k kutafuta uchumi. Viongozi wa Zanzibar badala ya kununua meli kubwa za uvuvi na usafiri na usafirishaji wanatumia hela nyingi kugharamia Ikulu, Mikoa mingi(vijimikoa), Wilaya nyingi(vijiwilaya), Tarafa, Kata na vijiji. Zanzibar inagharamia bunge na baraza la wawakilishi. Zanzibar ilitakiwa kujiendesha kama jimbo/mkoa maalum ndani ya Tanzania kwa kivuli cha Muungano na sio nchi ili kupunguza gharama zake za uendeshaji kama vimulimuli, mabenzi, kutunza wastaafu, mishahara ya Rais na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na watumishi wengine ndani ya kivuli cha "Zanzibar ni Nchi". Hata kama Zanzibar itajitenga, hali ya maisha ya wananchi wake haitaboreka kama inavyodhaniwa, badala yake Zanzibar itakuwa lango kuu la uhalifu kama vile biashara ya madawa ya kulevya, ushoga, na ugaidi. Kwasababu sioni kitu chochote kinachosababishwa na Muungano kinachoifanya Zanzibar isiwe na meli na viwanda vya mazao ya uvuvi, isiwe na meli za usafiri na usafirishaji, isiwe mzalishaji mkuu wa karafuu na mbata duniani. Badala yake Bakhessa ndiye mwenye meli za uhakika zinazotoka na kuingia Zanzibar.
Zanzibar Oyeee!!

Kwa hiyo?
 
Nakubaliana na wewe kwamba shida ya wanzanzibar si muungano bali ni maisha mazuri hilo halina mjadala, na wanzanzibar wamesubiri miaka mingi kuona maendeleo ndani ya muungano yanapatikana, lakini labda kwa utawala mbovu wa viongozi wa Zanzibar (ambao mimi naona ndio kikwazo) hilo halikutokea, ndio wakapeleka lawama kwa muungano (ambao hata mimi sioni tatizo la uwepo wake). Nakubaliana pia na hoja kwamba huenda maendeleo yasipatikane kwa namna ambavyo wanzanzibar wanaamini baada ya marekebisho ya serikali tatu. Ila nakataa kwamba ikitokea Zanzibar kujitegemea basi itakua ni kitovu cha maovu (madawa, ushoga na ugaidi) hili nakataa kwa sababu licha ya kwamba yote yapo hadi sasa hivi huko zanzibar lakini (wafanyayo hayo ni chini ya asilimia moja ya wanzanibar) nikimaanisha kwamba matendo hayo si utamaduni wa kizanzibar.... Nadhani nimeeleweka
 
Hizo meli za uvuvi n.k. mbona Tanzania ya muungano haina. Pili wazanzibar wengi kuwa nje ni ajili ya kipindi cha nyuma kuukimbia utawala wa awamu ya 1 ya nchi ile kwani ilikuwa si ya ki demokrasia sana na kwa watu wa Pemba waliona kama inawanyanyasa. Nchi nyingi zenye weusi nje ya nchi zao ni zaidi kwa ajili ya 1. haki za binadamu kama ifuatavyo: Wazanzibar - Awamu ya kwanza ya Zanzibar, waganda - Idi Amini, wanyarwanda - serikali ya wahutu ya post-independence Rwanda, wa angola - collaborators wa wareno walioukimbia uhuru, wa Ethiopia mchanganyiko wengine haile sellasie wengine haile Mariam, waghana - mapinduzi ya Nkrumah na serikali za kijeshi, wanaijeria - serikali za kijeshi n.k. 2. Uchumi - watanzania, walitafuta meli kupata pesa za kigeni na kwenda ulaya ili kurudi na vitu adimu, hali kadhalika wazimbabwe wakati wa Mugabe et.c. nchi za kusini kivutio ilikuwa SA ingawa apartheid iliwatisha. Migration na mobility za baadaye mpaka sasa ni globalization na free trade sasa wako wa halali na wahuni ndiyo imeletea mpaka madawa ya kulevya ambapo hatujui mwisho wake. Kwa hiyo unavyoziangalia population za foreigners nje ni mchanganyiko maalumu kwa mfano kuna wairani wengi sana japan na husingiziwa kila uhalifu unapotokea. Wale wamekimbia sharia kule iran et.c.
 
Watanganyika watakuwa omba omba zaidi kama zanzibr itajiondoa kwenye muungano,ufisadi,umalaya,uasherati,ukimwi,ujambazi,kuchunwa ngozi,udini,ukabila,kupigana mabomu na kuuwana vitashamiri sana,ingawa kwa sasa vipo kwa asilimia kubwa lakini vitazidi
 
Unahisi waTanganyika ndi wenye vitu hivyo tajwa hapo juu na waZenji hawana? Mwuvu ni mwovu tuu, be it mZenji, mTanganyika, hata mMbinguni kama ni mwovu ni mwovu tuu ndugu!
 
Wako Wazanzibar ambao wanadhani hali yao ya maisha itaboreka kama wakijitenga kutoka bara, mimi sidhani kama itakuwa hivyo. Tangu 1964 ya Muungano, Zanzibar ilipewa fursa ya kipekee ndani ya muungano ya kujiamulia mambo yake mengi yenyewe bila ya kuingiliwa na serikali kuu wala watu wa Tanganyika. Wazanzibar sio wengi ukilinganisha na wakazi wa Wilaya za Bara sebuse mikoa. Kutokana na hali ya kijografia ya Zanzibar ningetarajia Zanzibar ingekuwa kitovu cha uvuvi, usafiri majini na bandari kubwa nchini na Africa Mashariki lakini hili halikutokea na wala halitokei. Ukiwauliza wanasingizia Muungano. Wako busy na Zanzibar ni nchi, Zanzibar ni nchi kila siku na siku zote. Wazanzibar hawataki nchi bali wanachotaka wao ni maisha mazuri kiuchumi, na hii ndiyo inayosababisha wazanzibar wengi wametawanyikia Tanganyika, Dubai, UK, Emirates, n.k kutafuta uchumi. Viongozi wa Zanzibar badala ya kununua meli kubwa za uvuvi na usafiri na usafirishaji wanatumia hela nyingi kugharamia Ikulu, Mikoa mingi(vijimikoa), Wilaya nyingi(vijiwilaya), Tarafa, Kata na vijiji. Zanzibar inagharamia bunge na baraza la wawakilishi. Zanzibar ilitakiwa kujiendesha kama jimbo/mkoa maalum ndani ya Tanzania kwa kivuli cha Muungano na sio nchi ili kupunguza gharama zake za uendeshaji kama vimulimuli, mabenzi, kutunza wastaafu, mishahara ya Rais na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na watumishi wengine ndani ya kivuli cha "Zanzibar ni Nchi". Hata kama Zanzibar itajitenga, hali ya maisha ya wananchi wake haitaboreka kama inavyodhaniwa, badala yake Zanzibar itakuwa lango kuu la uhalifu kama vile biashara ya madawa ya kulevya, ushoga, na ugaidi. Kwasababu sioni kitu chochote kinachosababishwa na Muungano kinachoifanya Zanzibar isiwe na meli na viwanda vya mazao ya uvuvi, isiwe na meli za usafiri na usafirishaji, isiwe mzalishaji mkuu wa karafuu na mbata duniani. Badala yake Bakhessa ndiye mwenye meli za uhakika zinazotoka na kuingia Zanzibar.
Zanzibar Oyeee!!
"nakuhakikishia ndugu yangu, nje ya muungano na hawa ccm Zanzibar .... itakuwa ni nchi ya kupigiwa mfano, hoja uhai"
 
Nakubaliana na wewe kwamba shida ya wanzanzibar si muungano bali ni maisha mazuri hilo halina mjadala, na wanzanzibar wamesubiri miaka mingi kuona maendeleo ndani ya muungano yanapatikana, lakini labda kwa utawala mbovu wa viongozi wa Zanzibar (ambao mimi naona ndio kikwazo) hilo halikutokea, ndio wakapeleka lawama kwa muungano (ambao hata mimi sioni tatizo la uwepo wake). Nakubaliana pia na hoja kwamba huenda maendeleo yasipatikane kwa namna ambavyo wanzanzibar wanaamini baada ya marekebisho ya serikali tatu. Ila nakataa kwamba ikitokea Zanzibar kujitegemea basi itakua ni kitovu cha maovu (madawa, ushoga na ugaidi) hili nakataa kwa sababu licha ya kwamba yote yapo hadi sasa hivi huko zanzibar lakini (wafanyayo hayo ni chini ya asilimia moja ya wanzanibar) nikimaanisha kwamba matendo hayo si utamaduni wa kizanzibar.... Nadhani nimeeleweka

Mimi na mpinga mtoa hoja kuwa Zanzibar wakijitenga basi itakuwa kitivo cha maovu huo ni uongo wa mchana kweupe kwani wazanzibar ni watu wanaojiheshimu sana hata kutuzidi sisi watu huku bara kwani hata huku bara kuna maovu yote uliyo yataja hapo juu. Lakini pia naomba ujiulize wewe mtoa hoja huku bara kuna makaoo makuu ya jeshi la polisi, wananchi, na majeshi yote lakini kumekuwa kitivo cha uuzaji wa madawa ya kulevya na mengine yanapita mbele ya macho ya hoa polisi na yanakamatwa nje ya njee sasa unataka kusema kwamba nako bara wakijitenga na zanzibar watakuwa kitivo cha hayo maovu?
 
zanzibar ikijitenga amani ya kudumu itapatikana bara maana uovu wote hapa husababishwa na waislamu wa zanzibar
 
Kwa WaZanzibari hayo yooote uliyosema ambayo ndio changamoto zao, wao tafsiri yao ni huu Muungano!

Kwa sababu za kusingizia muungano basi wanataka hili na lile, yoote hayo, ya Baraza, ya Ubunge, ya mikoa ya wilaya, nk, yote ili wafanane na Bara, kama vile kuna ushindani!

Dhana kubwa waliyo nayo ni kujiona wanapunjwa ati kwa kuwa ni wachache/wadogo...

Waacheni wajitengenezee mipango yao labda watapunguza mambo mengine ambayo yanasukumwa na wivu tu!
Tatizo la Zanzibar ni huu muungano!
 
PHP:
[QUOTE][quote="mavumbi, post: 6912315"][COLOR=#ff0000][SIZE=3][FONT=comic sans ms]Kwa WaZanzibari hayo yooote uliyosema ambayo ndio changamoto zao,  wao tafsiri yao ni huu Muungano!

Kwa sababu za kusingizia muungano basi wanataka hili na lile, yoote hayo, ya Baraza, ya Ubunge, ya mikoa ya wilaya, nk, yote ili wafanane na Bara, kama vile kuna ushindani! 

Dhana kubwa waliyo nayo ni kujiona wanapunjwa ati kwa kuwa ni wachache/wadogo... 

Waacheni wajitengenezee mipango  yao labda watapunguza mambo mengine ambayo yanasukumwa na wivu tu!
Tatizo la Zanzibar ni huu muungano! [/FONT][/SIZE][/COLOR][/QUOTE]

[/QUOTE]

MAVUMBI: umemwelewa mtoa hoja lakini?

Anasema Wazenj wamezidiwa na tamaa za kupata mambo mengi ndio maana  hawana muda na muungano!
 
zanzibar ikijitenga amani ya kudumu itapatikana bara maana uovu wote hapa husababishwa na waislamu wa zanzibar
Sidhani kama kuna kiongozi yeyote wa harakati za kiislam Tanzania bara ambae ni mnzanzibar, hata hivyo idadi yao inasidiwa na waislam walioko bara na hata hapo Dar bado idadi ya waislam wanzanzibar ni ndogo kulinganisha na wazawa.
Kwahiyo hoja ya utulivu haina mashiko, kama waislam watakao baki hawata tendewa haki kama inavyolalamikiwa, basi shida iko pale pale, lakini usifikirie kwamba ni wengi ambao watarudi Zanzibar baada ya mabadiliko, ni wachache tu tena wale ambao huko bara wanaishi kwa kubahatisha. wenye shughuli zao hawataondoka na nadhani Mungu atatulinda ili isitokee GENOCIDE ameen..
 
Tatizo la Zanzibar sio hawataki Muungano ila hawataki UKOLONI maana Tanganyika wanaichukulia Zanzibar ni Koloni Lao na Si mshirika wa Muungano
 
Nawaunga mkono Wazanzibari wajiondoe kwenye Muungano kwani kujitoa kwao ndio kupatikana kwa Tangayika yetu.
 
Hakuna haja ya matusi. Tuachane kwa amani. Atakayekosa chumvi ataomba kwa jirani au kununua dukani!
That simple!
 
Wako Wazanzibar ambao wanadhani hali yao ya maisha itaboreka kama wakijitenga kutoka bara, mimi sidhani kama itakuwa hivyo. Tangu 1964 ya Muungano, Zanzibar ilipewa fursa ya kipekee ndani ya muungano ya kujiamulia mambo yake mengi yenyewe bila ya kuingiliwa na serikali kuu wala watu wa Tanganyika.

Wazanzibar sio wengi ukilinganisha na wakazi wa Wilaya za Bara sebuse mikoa.

Kutokana na hali ya kijografia ya Zanzibar ningetarajia Zanzibar ingekuwa kitovu cha uvuvi, usafiri majini na bandari kubwa nchini na Africa Mashariki lakini hili halikutokea na wala halitokei. Ukiwauliza wanasingizia Muungano.

Wako busy na Zanzibar ni nchi, Zanzibar ni nchi kila siku na siku zote. Wazanzibar hawataki nchi bali wanachotaka wao ni maisha mazuri kiuchumi, na hii ndiyo inayosababisha wazanzibar wengi wametawanyikia Tanganyika, Dubai, UK, Emirates, n.k kutafuta uchumi.

Viongozi wa Zanzibar badala ya kununua meli kubwa za uvuvi na usafiri na usafirishaji wanatumia hela nyingi kugharamia Ikulu, Mikoa mingi(vijimikoa), Wilaya nyingi(vijiwilaya), Tarafa, Kata na vijiji.

Zanzibar inagharamia bunge na baraza la wawakilishi. Zanzibar ilitakiwa kujiendesha kama jimbo/mkoa maalum ndani ya Tanzania kwa kivuli cha Muungano na sio nchi ili kupunguza gharama zake za uendeshaji kama vimulimuli, mabenzi, kutunza wastaafu, mishahara ya Rais na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na watumishi wengine ndani ya kivuli cha "Zanzibar ni Nchi".

Hata kama Zanzibar itajitenga, hali ya maisha ya wananchi wake haitaboreka kama inavyodhaniwa, badala yake Zanzibar itakuwa lango kuu la uhalifu kama vile biashara ya madawa ya kulevya, ushoga, na ugaidi.

Kwasababu sioni kitu chochote kinachosababishwa na Muungano kinachoifanya Zanzibar isiwe na meli na viwanda vya mazao ya uvuvi, isiwe na meli za usafiri na usafirishaji, isiwe mzalishaji mkuu wa karafuu na mbata duniani.

Badala yake Bakhessa ndiye mwenye meli za uhakika zinazotoka na kuingia Zanzibar.
Zanzibar Oyeee!!

Sasa kwanini Unamalizia kwa kusema ZANZIBAR OYEEE? kama hata BAHRESSA badala ya kuwajengea VIWANDA Mama vyenye Mali GHAFI za huko huko Zanzibar kama KARAFUU na SAMAKI... yeye kakimbilia ICE CREAM na Meli za Abiria za Kifahari kupeleka Watalii

Sasa ZANZIBAR OYEE ya nini???

Viongozi wengi wa Zanzibar wanaona ni Bora kushirikiana na nchi za ARABUNI lakini kwa sekta ipi? ELIMU? VIWANDA? UTALII?

au ZANZIBAR OYEE????
 
Kinachonipa mashaka ni kwanini watanganyika wanaacha kuijadili tanganyika yao itakuwaje wao wanaijadili zanzbr,vile visiwa watanganyika hamviwezi hata baba yenu nyerere vimemshinda kuvimeza,kiufupi ni kwamba utanzania ni uraia wa kuunga unga hauna mashiko bali utanganyika ndio asili yenu na wala haitotokea kusahaulika asili yenu hiyo,mujielewe hivyo.
 
Back
Top Bottom