Tatizo la Watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa na Mgongo wazi

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
575
2,559


Tatizo la watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa, au kuwa na mgongo wazi husababishwa na upungufu wa Folic acids anaokuwa nao mama mjamzito.

Mwongozo wa CDC unashauri kila mwanamke anayepanga kushika ujauzito aanze kutumia virutubisho hivyo walau miezi 3 kabla ili kuuandaa mwili wake vizuri katika kukabiliana na changamoto hizi.



Ikiwa folic acids zitatumiwa kwa kiasi cha 400 micrograms (mcg) kila siku, matatizo haya yatapunguzwa kwa zaidi ya asilimia 80.

Virutubisho hivi hupatikana kupitia vidonge maalumu vinavyouzwa kwenye maduka ya dawa, pia vinapatikana kwenye vyakula kama broccoli, spinach, vyakula jamii ya karanga, mayai, parachichi pamoja na samaki.

Ni muhimu pia kuendelea kutumia hata baada ya kupata ujauzito kwani hushirikiana na madini ya chuma katika kutengeneza damu mpya mwilini.

CDC
 
Elimu mzuri sana ,ila wanawake wengi wasomi hawatumii (kwa.ujinga wao)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…