SoC03 Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi: Foliki Asidi kwa Mama

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
MUHIMU KWA WAKINA MAMA WOTE WALIO KATIKA UMRI WA KUZAA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID MIEZI 3 KABLA YA UJAUZITO ILI KUZUIA ZAIDI YA MAGONJWA 100 IKIWEMO MGONGO WAZI NA KICHWA KIKUBWA.
FOLIKI ASIDI NI KOMAKOMA YA MIMBA

Folic acid naweza kusema ni moja ya kitu cha muhimu zaidi kwa mjamzito ambacho kitakuvusha kuelekea kujifungua mtoto mwenye afya njema zaidi. Inashauriwa kutumia kiwango cha microgramu 400 za folic acid kabla na baada ya ujauzito.Inasaidia kujifungua mtoto mweye afya njema ya ubongo na uti wa mgongo pia. Hakikisha unatumia kila siku kama ulivyoelekezwa hospitali

Folic acidi ni vitamin B ambayo inapatikana zaidi kwenye mboga za kijani na matunda yenye uchachu kama limau na chungwa. Lakini pia inaweza kutengenezwa maabara. Jina lingine la folic acid huitwa folate. Kazi kubwa za folic acid ikiwa ni kuimarisha uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu na pia ukuaji wa ubongo na uti wa mgongo kwa kiumbe cha tumboni.

WAKATI GANI WA KUMEZA VIDONGE VYA FOLIC ACID
Changamoto za kimaumbile hasa hutokea mimba ikiwa na week 3 mpaka 4. Kwahivo ni muhimu sana kuwa na kiwango kikubwa cha folate katika umri huu wa mimba. Ndio maana kuna umuhimu sana wa kupanga kushika mimba, ili kabla mimba haijaingia tayari uanze kumeza folic acid. Asidi ya foliki ina faida gani?
Bila kuwa na asidi ya foliki ya kutosha, dosari katika neva za fahamu na hivyo kuepusha kasoro za kimaumbile katika ubongo, mgongo na uti wa (neural tube defects). Magonjwa haya ni kama:

Spina bifida: Kutokukamilika ukuaji wa uti wa mgongo au pingili za uti wa mgongo.
Anencephaly: Kutokukamilika kwa ukuaji wa sehemu kubwa ya ubongo.
Watoto wenye “Anencephaly” mara nyingi hawaishi muda mrefu na wale wenye “spina bifida” huwa na ulemavu maisha yao yote. Habari njema ni kwamba kutumia nyongeza ya asidi ya foliki kipindi cha ujauzito inaweza kumuepusha mtoto wako kupata magonjwa haya kwa zaidi ya asilimia 50.

Kama utatumua kabla na wakati wa ujauzito, asidi ya foliki inaweza kumkinga mtoto wako dhidi ya:
 Mdomo sungura
 Kuzaliwa kabla ya muda (Njiti)
 Kuzaliwa na uzito mdogo
 Mimba kutoka
 Ukuaji dhaifu tumboni
 Asidi ya foliki pia inahusishwa na kupunguza hatari ya kupata:
o Matatizo kwenye ujauzito
o Magonjwa ya moyo
o Kiharusi
o Aina baadhi ya saratani
o Ugonjwa wa “Alzheimer”

VYAKULA VILIVYO NA FOLIKI ASIDI KATIKA KIWANGO KIUBWA NI KAMA:
• Mboga za majani kama spinachi, kabichi, loshu, broccoli
• Mimea jamii ya kunde kama maharage, mbaazi, njegere, njugu
• Karanga, njugumawe, nazi na korosho
• Matunda jamii ya sitrusi kama machungwa, machenza, limao.
• Nafaka zisizokobolewa
• Maini na Samaki
• Vyakula vilivyoongezwa foliki asidi.

IKumbukwe
Kichefuchefu, kupoteza hamu ya kula na kuvimbiwa ni madhara yanayoweza kutokea kwa mjamzito kama matokeo ya kutumia vidonge hivi. Ulaji wa chakula kidogokidogo badala ya kula milo mikubwa mitatu kwa siku, kula na kunywa taratibu na kufanya mazoezi mepesi mara kwa mara yanaweza kusaidia dalili hizi unazoweza kupata kama matokeo ya kutumia asidi ya foliki. Ikiwa dalili hizi zinaendelea kuwa mbaya, wasiliana na daktari/mkunga anayesimamia maendeleo ya ujauzito wako mara moja.

Mtoto tumboni yuko katika hatari ya kupata dosari katika mfumo wa fahamu ikiwa: mama mjamzito aliwahi kupata ujauzito ulipata dosari katika mfumo wa neva za fahamu, wewe au mwezi wako ana kasoro katika neva za fahamu aliyozaliwa nayo,katika familia yako au mwezi wako kuna historia ya watu kuzaliwa na dosari katika neva za fahamu, mjamzito ana kisukari,mjamzito ana uzito mkubwa uliopitiliza na mjamzito ana ugonjwa wa siko seli.

Mama ambaye hakutumia foliki asidi kabla au miezi ya awali ya ujauzito ajadiliane na daktari/mkunga anayesimamia maendeleo ya ujauzito wake, wataweza kukushauri nini kifanyike na dozi kiasi gani itumike kuokoa maisha ya mtoto tumboni. Tafadhali usitumie dawa hizi mwenyewe bila kujadiliana na daktari kwanza.
Kichwa kikubwa(maji katika ubongo)maji hayo yapo kama ute yanayozunguka ubongo na uti wa mgongo.

HALI YA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI TANZANIA
Hakuna takwimu halisi inayoelezea idadi ya Watoto wanaozaliwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi ila kutokana na takwimu iliyofanywa muhimbili takribani watoto 1000 wanaozaliwa kila siku nchini watatu wanazaliwa wakiwa na matatizo ya ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi idadi ambayo imeelezwa kwa mwaka inafikia watoto 4840

HALI ILIYOPO YA MATIBABU
Matibabu ya kichwa kikubwa ni aidha VP SHUNT(mpira wa maji kwenye kichwa utaopitisha maji kwa njia ya mkojo)au ETV.Ingawa Tanzania tunatumia VP Shunt ila kiwan Matibabu ya kichwa kikubwa ni aidha VP SHUNT(mpira wa maji kwenye kichwa utaopitisha maji kwa njia ya mkojo)au ETV.Ingawa Tanzania tunatumia VP Shunt ila kiwango cha Watoto kufa kinaongezeka na inasumbua sana wakati wa matibabu yake.Kwasababu ya bei kubwa ya VP Shunt na gharama za kimatibabu,uhaba wa wataalamu wa upasuaji ,kwa Tanzania hospitali saba zinafanya upasuaji wa mgongo waz na kio cha Watoto kufa kinaongezeka na inasumbua sana wakati wa matibabu yake.Kwasababu ya bei kubwa ya VP Shunt na gharama za kimatibabu,uhaba wa wataalamu wa upasuaji ,kwa Tanzania hospitali saba zinafanya upasuaji wa mgongo waz na kichwa kikubwa ambazo ni MOI,Bugando,MZRH,Ndanda,Seliani Hydom na KCMC katika hizi hospitali MOI na BMC ndizo zinapokea wagonjwa wengi na zinafanya upasuaji huo mara zote ivyo inawalazimu wamama na Watoto wao kusafiri umbali mrefu ukizingatia wengi wao ni wakazi wa vijijini na ambapo ni mbali na huduma hizo.

akati umefika jamii kuacha kuwa na mila potofu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na dhana hiyo ianze kwa wazazi, walezi na familia inayowazunguka. “Kwani imani potofu ndio zimepelekea wazazi na walezi wa watoto hao kutumia fedha nyingi kwa waganga wa kienyeji bila mafaanikio na kusababisha ongezeko la vifo vya watoto wao”Alisema Waziri Ummy wakati wa maadhimisho ya kichwa kikubwa na mgongo wazi.

PENDEKEZO
Tanzania ijenge kiwanda cha VP SHUNT, CATHETERS, IRYFEX CONE NA mifuko ya ENEMA kuepuka vifo vya Watoto hawa.

BAADHI YA PICHA HAPA CHINI ZINAZOONYESHA WATOTO WALIOZALIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI SABABU KUU NI WAKATI WA MAANDALIZI YA KULETWA KWAO DUNIANI

Screenshot_20230510_145345_Microsoft%20365%20(Office).jpg
InShot_20230510_184507961.jpg
InShot_20230510_184715233.jpg
View attachment picha za watoto walioathiriwa tangu mimba.docx
 
Attachments

  • picha za watoto walioathiriwa tangu mimba.docx
    771.6 KB · Views: 9
  • picha za watoto walioathiriwa tangu mimba.docx
    771.6 KB · Views: 5
  • picha za watoto walioathiriwa tangu mimba.docx
    771.6 KB · Views: 2
  • picha za watoto walioathiriwa tangu mimba.docx
    771.5 KB · Views: 1
  • Folic acid-1.docx
    925.4 KB · Views: 3

View attachment 2616955View attachment 2616958View attachment 2616963View attachment 2616966
Watoto wanapata madhara makubwa sana kwa kuchelewa kupata huduma, kwa utafiti uliofanywa kwa Watoto zaidi ya 3800 unaonyesha chini ya 20% wamefanyiwa upasuaji chini ya umri wa miezi 6, kwa mantiki hiyo endapo mtoto akifanyiwa upasuaji kwa muda huo kutakuwa na matokeo chanya.

1Uchunguzi wa 2018-2022 kwa Watoto 3800, 20% walifanyiwa upasuaji chini ya miezi 6, nakathalika 80% walifanyiwa upasuaji wakiwa Zaidi ya miezi 6, hivyo walifanyiwa upasuaji wakiwa wamechelewa.
-Umbali wa vituo vya kutolea huduma
-Uchumi kwa mzazi au mlezi wa mtoto
-uwelewa kwa watoa huduma wa afya na wananchi.
Baada ya kuchunguza gharama za matibabu, hospitali ya Bugando ilithibitisha kupokea Watoto kati ya 40-50 kwa mwezi, ambapo ni sawa na makadirio ya Tsh. 40,000,000 hadi 50,000,000 kwa mwezi. Huduma ya matibabu kwa mtoto mmoja ni Tsh. 1,288,333

-Lab- Ultra sound
-Surgery
-Wodini
-Supplies
-Equipment
-Scrub
-Gauze
Ni ngumu sana kwa mzazi wa kitanzania kumudu na ukizingatia wengi wao ni waakina mama masikini na watoto waliozaliwa kwenye familia za chini kabisa na hata uwezo wa kulipia bima bado ni kizungumkuti.
 
Ni kweli kaulimbiu ilikuwa ni uwajibikajina uwajibikaji kuanzia mtu binafsi serikali mpaka taifa kwa ujumla...

Serikali kutokana na kamusi ya kiswahili inasema ni mamlaka,ni watu na taasisi ndani ya jamii hasa dola yenye mamlaka ya kutawala na kufanya maazimio kwa wote katika eneo fulani.
Ndio maana andiko linatoa rai kwa jamii,serikali na watu binafsi walau Tanzania tuzalishe vifaa vyetu wenyewe kusudi watoto wasikawizwe au kucheleweshwa kupata huduma kwa wakati sababu ya Shunt...
Pia elimu ya kutosha inapaswa kuwepo kusudi wamama wanapokuwa wajawazito kutumia vyakula vyenye Folic Acid vikiambatana na vidonge vya Folic Acid kuepuka watoto wenye mapungufu wazaliwapo kupelekea ulemavu wa kudumu.
 
Back
Top Bottom