Wadau, kumekuwa na tatizo la umeme lililopindukia hapa Tanzania, kiasi cha kutia aibu. Haiwezekani nchi yenye rasilimali zote muhimu kwa ajili ya kuzalisha umeme kuwa na mgao wa saa 24. (Kuanzia saa mbili asubuhi siku ya kwanza, mpaka saa mbili asubuhi siku ya pili), tena kimyakimya. Lakini pia kuna kipindi serikali ilitangaza kuwa suala la mgao litakuwa ndoto. Hivi kweli tuko makini? Ok. nini kifanyike?