Tatizo la umeme mpaka lini?

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,594
9,338
Wana jf, huku mbezi usiku huu tanesco wamekata umeme, sasa nahisi tumefika pabaya, hapa ni joto hapalaliki. What the hell is this!
 
Maeneo mengi tu hayana umeme. Watu kutoka Arusha, Mwanza, mbeya, Iringa, Kibaha, na Moro wamearifu kuwa pia maeneo hayo yamekatiwa power. Dharura ya aina hii ya kukatika kwa umeme maeneo meng ya nch wakat wa usiku inatokea kwa mara ya 2 toka walipotangaza kuwa mgao umepungua. Hyo ni mbali na ile kata kata ya vipindi vifupi vifupi bila taarifa wanayofanya mchana..dah, tunanyanyasika, nch gan inaongozwa kwa mipango ya dharura hii yarabi!!!
 
kaka grid imepiga chini nchi nzima lkn tatizo litaisha tu siku akiingia mpangaji mwingine pale magogoni
 
ah! Walah hebu hata uso wa aibu tu! Tatizo la umeme miaka yote! Du! Jamaa makauzu kwelikweli.
 
Nchi za wenzetu ungekuta asubuhi waziri anaomba radhi na kung'atuka, mkurugenzi nae anafata, injinia mkuu nae hvyohvyo sasa huku kwetu ndo kwaaanza bodi mpya imewekwa! Zisi izi veri disturbing.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nchi za wenzetu ungekuta asubuhi waziri anaomba radhi na kung'atuka, mkurugenzi nae anafata, injinia mkuu nae hvyohvyo sasa huku kwetu ndo kwaaanza bodi mpya imewekwa! Zisi izi veri disturbing.

Mpaka siku magamba watakapong'olewa madarakani, lakini kwa kuwa wameshagundua namna ya kuchakachua chaguzi sijui kama hili litatokea bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.
 
Kinachonifurahisha ni jinsi tunavyojua kuongea na kulalamika, ila vitendo a a! Hii ni kutokana na sera zetu nzuri za utulivu na amani! Na ukiandamana kwa amani unatafuta uvunjifu wa amani, Unajua nani hao wanoongoza kwa kuvunja amani wakati inapotafutwa?
 
Na vitengo vya magamba alias vyombo vya dola vimeshapata kisingizio cha shambulizi la kigaidi kutoka katika lile kundi la kihuni la Wasomali ndiyo imetoka hiyo maandamano ni "MARUKUFU"....Juzi walidai kulikuwa na uwezekano wa shambulizi katika mechi ya Yanga na Simba na pia kwenye maandamano ya kupinga malipo ya DOWANS. Cha kushangaza wakaruhusu mechi ya Simba na Yanga ichezwe lakini wakaweka ngumu kwenye maandamano!!!
 
Back
Top Bottom