Tatizo la simba ni Friends of Simba

Tatizo la simba ni Friends of Simba

Mahweso

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
1,098
Reaction score
1,501
Natoa lawama zangu moja kwa moja kwenye kundi hili kutokana na mambo yao, kiburi, Dharau na kejeli walizo zitoa wakati wa uchagu mkuu wa Simba SC, kama ulikuwa mfuatiiaji mzuri wa uchaguzi ule utajua kuwa kulikuwa na matatizo gani na Ndumbalo alitumuka vipi kuvuruga uchaguzi ule, Maneno ya kuwaita wanacham wengine maskini hawana pesa za kuendesha Club na kuifanya kuwa na maendeleo.

Hayo tuyaache. Kubwa ni hili la Club kufanya vibaya, kama ujuavyo mpira ni Umoja, Fitna, majungu na uchafu mwiiiiingi sana ili kufanikisha lengo la timu kushinda au kupata maendeleo. Sasa hawa Friends of Simba wameyaua yote haya, hakuna umoja katika Club, kwahiyo yale yooote niliyoyasema wanayafanya wao kama wao,fitna, majungu na uchafu mwingine wanaufanya wao kama wao. Simba haijaanza leo tunajua, wapo wazee wanajua mbinu na majungu na njia ili timu ifanye vizuri kwani kuna mtu haijui Africa?

Hujuma katika timu, Friends of Simba wasilalamike haya waliyaanza wao kipindi cha Rais Rage, waliwatumia tawi la Mpira Pesa kuvuruga na walikuwa wanawatumia wachezaji kuhujumu na kama mnakumbuka kipindi cha Kocha Mfaransa Simba alibadirisha kikosi kizima na kuanza kutumia Vijana na kama mnakumbuka Rage alipata upinzani mkubwa sana kutoka kwao mpaka kuaanda mapindizi ambayo yalifeli kutoka na uimara wa watu waliokuwa nyuma ya Mh:Rage,

Sasa kama kweli mna fikra na kumbukumbu hawa wachezaji wanao sumbuliwa sasa walikuwa ni wachezaji wazuri sanakipindi cha uongozi wa MH: Rage, kitugani kimeacha wawe wabovu na wengine kufukuzwa?

Jibu ni moja, walikataa kutumika na ndio maana Tambwe anaanzia bench, Musoti kutimuliwa, Edward Christopher kukimbilia Polisi, Chanongo na Kiemba kuhisiwa wanahujumu sababu walishindwa kuwasikiliza kipindi kile cha Rage.

Oooo ukawa, ukawa walitakiwa wasikilizwe tu kama walivyo sikilizwa Mpira pesa kiburi hakisaidiii
Mwisho, asiye amini nuchawi Africa basi yeye ni mchawi anaewafumba macho wengine wasijue mafanikio yake,
Mpirani uchawi upo, Maofisini uchawi upo, bila uchawi kusinge kuwa na Maombezi ya kutoa mambo ya giza, giza ni nini? si uchawi?
Friends of Simba kaeni pamoja na wanachma wenu mliowaita maskini muyamalize mpira uchezwe, maana mmesema timu ni yenu na ukiangalia Kuanzai Rais hadi watendaji wote ni Friends of Simba, lekebisheni hili
 
Definetly, wakae wayamalize... Tunaoumia ni sisi mashabiki/wapenzi wa simba... Otherwise tuta wa Burkina Faso
 
"Vita vya panzi ni furaha ya kunguru"....
 
Mpira wa Tanzania hauwezi kundelea mpaka watu wenye njaa waondolewe kwenye vilabu.
 
Mpira WA bongo vituko Sana unaweza kuta hyo anayosema mleta mada hana ushahidi hta mmoja kayaokota vijiweni kaleta km yalivyo
 
Friends of Simba turned into enemies of Simba
 
Back
Top Bottom