Hakuna namna uozo kama unaotokea Tanzania unaweza kuisha kwa watu kufikiri kuwa kuna "chama" au "mtu fulani" ndio chenye/mwenye uwezo wa kuweka mambo sawa. Hiyo ni nje kabisa ya kanuni kuu ya demokrasia. Kwanza, tujiulize ni kitu gani hasa kilisababisha binadamu hapo awali kufikia kuhitaji demokrasia katika mifumo yao ya uongozi na utawala? Ni kitu kilicho wazi kabisa kwamba, binadamu ana mapungufu na hawezi kutegemewa kutenda sahihi na haki wakati wowote. Mienendo na tabia za binadamu hazina "guarantee" yoyote. Kwa asili, binadamu wengi wakiaminiwa kupita kiasi na kukabidhiwa mamlaka yasiyo na ukomo, hujenga jeuri, dharau na kiburi kisichomithilika.
Jibu pekee ni kuweka demokrasia ya kweli inayowawezesha wananchi kuwajibisha vyama na viongozi wasipotimiza wajibu wao. Kuwafanya wawe na "hofu" ya "kauli ya umma" kama vile tunavyotakiwa kuwa na "hofu" ya Mungu. Hii kushabikia kutawaliwa na "messiah" na kundi la "mitume" wasiohojiwa hapa duniani ni ujinga uliopitiliza. Lazima tufikie mahali ambapo tunaenda kwenye chaguzi bila kuwa na uhakika wa chama kipi au mgombea yupi atashinda au kushindwa. Tatizo ni CCM? Wape guarantee hiyo hiyo CHADEMA/CUF/ACT kuwa madarakani bila kikomo kama hujaona uozo ukiendelea kama kawa.
Aidha, Rais hatakiwi kuwa na kauli ya mwisho kwenye maamuzi makuu ya kitaifa na katika teuzi/tengua za nafasi kwenye taasisi nyeti za dola. K.m. Marekani, Trump hawezi kumfukuza kazi (kumtumbua) hata mtendaji wa forodha bandarini kwa kuamuru tu akijisikia kuudhiwa. Hapa kwetu rais akisema, ndio mwisho wa yote; hahojiwi wala sheria haiuliziwi. Yakiharibika ndio anakimbilia kudai ushirikiano na uzalendo wa wote kurekebisha makosa yake. Katiba makini is the right starting point. Kenya ni mfano kiasi chake. Rais Kenyatta anatamani kufanya fujo lakini tayari amedhibitiwa na mfumo - hana janja zaidi ya kuanzisha machafuko.