Emmanuel J. Buyamba
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 1,167
- 651
Tokea kuanza kusomwa hadharani ripoti mbalimbali za kamati za uchunguzi wa madini, kumeibuka tafsiri ya kwamba wasomi wetu hawalisaidii taifa. Kwa upande wangu huu mtazamo nauona hauko sawa.
Tatizo la nchi hii muda wote lipo kwenye mfumo mbovu unaolelewa na katiba mbovu ya nchi.
Leo kiongozi mwandamizi anaulizwa kwa nini ulisaini hizo nyaraka anajibu niliagizwa na bwana mkubwa ambae ndiyo aliyemteua. Na kwenye katiba huyo bwana mkubwa unakuta hahojiwi wala hashitakiwi mahakamani kabla na baada ya kustaafu.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amefikia mahala akawaita majaji waliotengua ushindi wake kuwa ni "wakora" hali inayoonesha kuwa anachuki kali kifuani ila kwa kuwa mfumo ndiyo uliowapa majaji wale uhalali, amebaki kuugulia maumivu moyoni.
Kina professa Lipumba na wenzake nao wanafanya mambo ya hovyo leo hii kwenye chama walichofukuzwa kwa sababu tu ya mfumo mbaya wa baadhi ya vyombo vya serikali kujiingiza kwenye vyama vya siasa.
Hata hawa CCM ambao tunawaona hawafai ni kwa sababu ya system mbovu inayowapa "umungu mtu" fulani hivi wa kutenda wanavyojisikia.
Kwa hiyo ndugu zangu badala ya kuwashambulia wasomi wetu hebu hizo nguvu tuzielekeze kwenye kupigania mfumo bora wa kiuongozi.
Sote tuseme tunaitaka rasimu ya Jaji Warioba irejeshwe kwa wananchi,ijadiliwe na tupate katiba mpya!!