Kama kuna kitu kitanihamisha tabata ni maji sidhani kama manispaa ya ilala ina mipango yoyote ya kutatua kero ya maji katika manispaa yake.
Jana wametupatia maji baada ya wiki moja kupita. Je wastani wa matumizi ya maji Tabata na kwingineko kwenye mgao kama wetu ni mara moja kwa wiki? Hizi siku nyngine mnategemea tunatumia nini? Hata kama mnadhani tuna vyombo vya kutosha kuhifadhia maji, ina maana kwa sisi wapangaji inabidi niongeze chumba kingine cha kuweka ndoo za maji. Maji ni lazima na haki ya msingi. Tunataka maji kila siku walau kwa saa moja.Maji kwetu hutolewa mara DAWASCO wanapojisikia na inavyowapendeza. Mwezi huu tumepata maji mara moja na nusu. Ile ya kwanza yalitoka kwa dakika takriban 50' na baada ya wiki mbili na nusu wiki iliyopita yakatoka kwa dakika kama 20 na kwa pressure kama vile mtu anapomalizia kukojoa mkojo wa mwisho. Tatizo hili ni bahati mbaya au makusudi? Kwa wale wenye visimi vya maji biashara wanafanya kweli! Hapo hakuna syndication kweli?
DAWASCO Tabata.......kwanini mabomba ya mchina hayatoi maji eneo la Chama Mawenzi?. Juzi kati tumechanga fedha kununua bomba kurudishia lillokatwa tunaambiwa eti Meneja kahamishwa tusubiri...
Kwani Mbunge wa eneo hili ni wa chama cha "upinzani"?Kaka maeneo Mengi ya Tabata yaani kuanzia Liwiti, Baracuda, Mangumi, Chama, Segerea, Kisukuru, Kinyerezi kiukweli yana mtandao wa mabomba ya maji lakini yanahujumiwa ili maji yasitoke. Tangu mwaka 2002 sijawahi kuona maji ya bomba tabata hii hii ya Makongoro Mahanga. nilishazoea maji ya chumvi na kuoga lazima utumie sabuni ya magadi toka kigoma. Hii ndio Dar et