Tatizo la maji tabata ni halisi?

Tatizo la maji tabata ni halisi?

Jahom

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2008
Posts
351
Reaction score
32
Maji kwetu hutolewa mara DAWASCO wanapojisikia na inavyowapendeza. Mwezi huu tumepata maji mara moja na nusu. Ile ya kwanza yalitoka kwa dakika takriban 50' na baada ya wiki mbili na nusu wiki iliyopita yakatoka kwa dakika kama 20 na kwa pressure kama vile mtu anapomalizia kukojoa mkojo wa mwisho. Tatizo hili ni bahati mbaya au makusudi? Kwa wale wenye visimi vya maji biashara wanafanya kweli! Hapo hakuna syndication kweli?

Tangu nilipowasilisha, hatujapata maji tena. Walileta bill yao nidhani nikilipa wataanza kutoa maji kila siku. jana nilimuona Waziri wa Maji anasherehekea wiki ya Kutokuwa na maji, kwa hakika maji si mahitaji ya msingi
 
Kweli kumbe Tabata hakuna watu Bali wahamiaji feki
 
Wahamiaji feki wa Tabata hawaoni tabu kukosa maji
 
Kuna tatizo la msingi kwenye JF, threads zote hazina maoni ya kutosha. Kindly review the policy
 
Watu wangu vipi kuhusu tatizo la mgao usiojulikana na ratiba maalum?
 
Tatizo ni kubwa mkuu tangu November maji yametoka last week...Nilikwenda DAWASCO kuuliza nikaambiwa mtambo unaoleta maji Tabata una matatizo
 
leo asubuhi nimeacha yanatoka,mpaka gari nimesafishia maji ya dawasco
 
Nashukuru kwa taarifa, nilitoka kidogo sipo Tabata. Hoja kuu ni ratiba na kutopeana taarifa rasmi ya iwapo kuna tatizo na lini litatatuliwa kama wanavyofanya kwa mitaa ya Masaki, Oysterbay na baadhi ya maeneo nyeti. Tabata na baadhi ya maeneo ya line hiyo hatujui kinachofuata.
 
Kwan hua kuna ratiba ya kutoa maji?? Cku zipi kwa wiki??
 
Imekuwa ni kero kwa kweli mpaka wajisikie ndo wafungulie maji
 
Kama kuna kitu kitanihamisha tabata ni maji sidhani kama manispaa ya ilala ina mipango yoyote ya kutatua kero ya maji katika manispaa yake.
 
Kama kuna kitu kitanihamisha tabata ni maji sidhani kama manispaa ya ilala ina mipango yoyote ya kutatua kero ya maji katika manispaa yake.

Kuna Mtaa unaitwa Chama Mawenzi, maji hayajawahi kutoka mwaka wa nane huu. Wachina walipotandaza mabomba wauza maji wakachanga mlungura ukaenda DAWASCO main bomba likakatwa.
 
Maji kwetu hutolewa mara DAWASCO wanapojisikia na inavyowapendeza. Mwezi huu tumepata maji mara moja na nusu. Ile ya kwanza yalitoka kwa dakika takriban 50' na baada ya wiki mbili na nusu wiki iliyopita yakatoka kwa dakika kama 20 na kwa pressure kama vile mtu anapomalizia kukojoa mkojo wa mwisho. Tatizo hili ni bahati mbaya au makusudi? Kwa wale wenye visimi vya maji biashara wanafanya kweli! Hapo hakuna syndication kweli?
Jana wametupatia maji baada ya wiki moja kupita. Je wastani wa matumizi ya maji Tabata na kwingineko kwenye mgao kama wetu ni mara moja kwa wiki? Hizi siku nyngine mnategemea tunatumia nini? Hata kama mnadhani tuna vyombo vya kutosha kuhifadhia maji, ina maana kwa sisi wapangaji inabidi niongeze chumba kingine cha kuweka ndoo za maji. Maji ni lazima na haki ya msingi. Tunataka maji kila siku walau kwa saa moja.
 
DAWASCO Tabata.......kwanini mabomba ya mchina hayatoi maji eneo la Chama Mawenzi?. Juzi kati tumechanga fedha kununua bomba kurudishia lillokatwa tunaambiwa eti Meneja kahamishwa tusubiri...
 
DAWASCO Tabata.......kwanini mabomba ya mchina hayatoi maji eneo la Chama Mawenzi?. Juzi kati tumechanga fedha kununua bomba kurudishia lillokatwa tunaambiwa eti Meneja kahamishwa tusubiri...

Kaka maeneo Mengi ya Tabata yaani kuanzia Liwiti, Baracuda, Mangumi, Chama, Segerea, Kisukuru, Kinyerezi kiukweli yana mtandao wa mabomba ya maji lakini yanahujumiwa ili maji yasitoke. Tangu mwaka 2002 sijawahi kuona maji ya bomba tabata hii hii ya Makongoro Mahanga. nilishazoea maji ya chumvi na kuoga lazima utumie sabuni ya magadi toka kigoma. Hii ndio Dar et
 
Kwani Mbunge wa eneo hili ni wa chama cha "upinzani"?
 
Hamieni huku, sie hajui kama kuna matatizo ya maji nchi hii
Ila umeme lol! Muongo anaukata kila anapojisikia
 
maji kutoka maeneo yetu ni mpaka wenye visima washibe hela ndiyo DAWASA wanafungua kwa dakika tano. Kuna wafanyakazi kila siku wanaenda kazini DAWASCo kukaa eti wanatoa huduma kwa wateja wa kukusanya malipo ya bill bila huduma yenyewe na wafurahi wanapoona tunalipa bila huduma. Kumbe tunalipa kwa kudhani wataanza leo, kesho, kesho kutwa ..............?????????????????? F...You!!!!
Tabata tuna miezi miwili kamili bila maji na jamaa ofisi yao infunguliwa kila siku. Napata hasira za kuwalipua!!!!!! Halafu waziri wa maji ndo anapanda jukwaani kusherekea siku ya kukosa maji, timamu iko?????? Nina hasira kwa kuwa hata taarifa ya tatizo hazisemwi, na tatizo halina ukomo ili tuishi kwa matumaini. Pambafu!!!!
 
wiki ya maji dar, msituonyeshe mnatutia uchungu!!!!
 
Back
Top Bottom