Tatizo la maji kwa Watanzania ni ufinyu wa fikra za watanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,173
Moja kati ya vituko vya Tanzania, ni Tanzania hubaki na shida ya maji baada ya shida ya mafuriko.
Tanzania ina miji yenye maji mengi kiasi cha kuweza kuua watu kwa mafuriko kila mwaka. Kuwa na mvua za kutosha zenye kuleta mafuriko pia.

Zaidi ya kuwahamisha watu au kuwatahadharisha watu kukaa katika maeneo hatarishi, hakuna mwenye mpango wa kufanya hatari ya mafuriko kuwa fursa. Kwa upande wangu nimeona, tunaweza kuyaelekeza maji katika maeneo tunayoyataka ili kuzuia mafuriko, na katika kiangazi tukatumia maji tulioyahifadhi ili kuwapatia raia maji safi na salama kwa mwaka mzima bila shida.

Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuleta kauli ya kutunza vyanzo vya maji, kiasi cha kuwahamisha watu maeneo ya milimani, na kuwaleta maeneo yasiyo na maji bila kuandaa miundo mbinu ya kuwapelekea maji maeneo wanayowahamishia.

Na hata ikiwa kuna miundo mbinu maji huwa ni shida kwa kuwa miundo mbinu hiyo hupitisha hewa badala ya maji. Shida imekuwa mara mbili, wakati wa mvua watu hulalamika maji (Mafuriko), wakati wa kiangazi watu hulalamika kukosekana kwa maji. Kituko.

Dhana yetu dhidi ya mafuriko ipo kwa upande mmoja, na ndio huzaa tatizo lingine. Mafuriko yakichukuliwa kama chanzo kikuu cha maji, shida ya maji haitakuwepo, badala ya kuliona hili watendaji huona mafuriko ni janga lisilo na faida ndani yake.

Baada ya kuona mafuriko kuwa janga, tumekuwa tukilikwepa. Ni akili finyu pekee ndiyo inapaswa kutegemea vyazo vya asili vya maji, kwa kuwa vyanzo hivyo hupunguza uwezo wa kutoa maji wakati wa kiangazi hivyo maji huwa shida, hapo ndipo mtu ilibidi afikiri namna ambayo angeyahifadhi maji ya mafuriko ambayo kwa akili za woga aliyakimbia na kukosa namna ya kuyafanya.

Sisemi kwamba tusiepushe vifo vinavyotokana na mafuriko, ila baada ya kukwepa mafuriko tuangalie namna ya kuyafanya maji hayo yatakavyotusaidia wakati wa kiangazi. Ni kawaida kwa mamlaka za maji kusema kuwa uhaba wa maji unaotokea kipindi cha kiangazi ni matokeo ya kupungua kwa maji katika vyanzo husika. Ni jibu sahihi, ila linatokea kila mwaka, je nini hufanyika ili kufanya hata maji yakipungua katika vyanzo vyake, hakutakuwa na mwananchi atakayepata shida ya maji?

Hapa ndipo kituko kilipo, katika hili huwa napenda kuchukua mfano wa mkoa wa Morogoro. Katika wilaya ya Kilosa, ni kila mwaka maji huleta tabu hasa maeneo ya Dumila ambapo kuna eneo wameamua kuliita ferry kwa kuwa hufurika sana wakati wa mvua. Yapo maeneo mengi ya milimani ambayo pia huwatesa raia kwa mafuriko, ni katika mkoa huo huo wa Morogoro ambao kuna maeneo hayana maji kabisa na wala sidhani kama kuna mpango wa kupeleka maji.

Serikali inayojisifu kuleta maisha bora hujisifu kwa miradi ya waarabu ambao huwachimbia visima wananchi wa kijijini. Hii ni sawa na mtu kukodi gari kuanza kujinadi kuwa gari ni lake. Kujisifu kwa misaada.

Katika fikra sahihi, tunaweza kuyafanya maji ya mafuriko yasiwe na tabu kwetu ila yakatusaidia wakati wa kiangazi. Ubaya ni fikra. Nchi kama Tanzania yenye mito mingi inayofurika kila mwaka, sio nchi ya kukosa maji hata kwa mikoa iliyo katika maeneo ya nusu jangwa kama Dodoma, ni namna ya kusambaza maji kutoka katika maeneo mbalimbali.

Labda ni uvivu au kutokuwa tayari. Nasema tatizo ni fikra. Huwezi kutegemea SDG’s kutatua tatizo lako ambalo liko ndani ya uwezo. Ndio hao na sera zao za kuleta maisha bora tangu wakati MDGs wameleta matatizo ambayo bado wengi hatujayajua kuwa ni matatizo.

Uhuru wa kweli ni fikra. Sisi wengi hatuna kazi na fikra. Tumekuwa na tabia za zamani, kuwa mkarimu kwa mgeni kuliko kwa sisi wenyewe. Hoteli za kitalii zina maji hadi wanayamwaga kwa urembo kwenye ‘fountains’ wakati kuna mwananchi ambaye japo ana bomba la maji nyumbani kwake mwezi mzima maji ananunua. Maji yamewezaje kutoka yalikotoka yakafika kwenye hoteli hizo? Nataka kusema kuwa, uwezo wa kuyasafirisha maji na kufika tunapotaka yafike tunao.

Tuyape sura mpya mafuriko. Tuyafanye kuwa fursa na sio kuona kama ni tatizo la kutolihitaji. Fikra ya ukombozi ni ile inayoangalia matatizo kama fursa na kaweza kuitumia. Hapa ni fikra ndogo sana inayohitajika, kama kuku tu katika uchafu hakosi cha kumshibisha. Tanzania katika mafuriko haipati maji ya kunywa hata kuku ametushinda katika hili.



Muandishi wa makala haya anakaribisha mjadala.
Wasiliana naye kwa simu 0718651585
 
Nimekuelewa ndugu Analogia Malenga. Tunaweza kutumia maji yatokanayo na mafuriko kama sehemu ya vyanzo vyetu vya maji hasa wakati wa kiangazi.

Zipo nchi zilizofanikiwa katika hilo na wao hawakusanyi tu maji ya mafuriko bali runoff yoyote inayokuwa generated wakati wa mvua mfano ni Namibia. Upo utaalam unaotakiwa kuwezesha hilo lakini pia fedha kwa ajili ya study ya namna hiyo pamoja na ile ya kujenga miundo mbinu yake.

Utayali wa serikali kwenye project za namna hii ungesaidia kwa kiwango kikubwa hasa kwa maeneo kame kama Dodoma lakini pindi yapatapo mvua basi tunashuhudia maji mengi kama runoff na mwisho hutoweka baada ya siku chache na hivyo kutuacha na tatizo lile lile la uhaba wa maji.

Maji yanayozalishwa kule kwenye visima vya Mzakwe kamwe hayatakaa yatosheleze mahitaji ya maji kwa mji wa Dodoma na hasa kwa siku za usoni ambapo mji unakua na mahitaji kuongezeka. Alternative source ya maji iliyoandaliwa ni ipi? Zipo techniques za kutumia ili kuweza kufanya flood mapping kwa maeneo yote unayotaka.

Na unaweza kwenda mbali kwa kuangalia kiasi cha maji unachoweza kukusanya na hivyo ukafikiria jinsi ya kuhifadhi maji hayo iwapo bado kwa eneo hilo yatasaidia zaidi. Lakini kulingana na uhifadhi wako unaweza kuhifadhi maji hayo mwaka huu yakakusaidia labda kiangazi cha miaka 5 ijayo.

Hauyapotezi. Swali ni je serikali yetu ipo tayari kuwekeza kwenye tafiti hizo? Na je ipo tayari kuinvest kwenye project hizo? Au tuendelee kuona mafuriko, tupoteze maisha na mali za watu.

Lakini pia tuyapoteze maji hayo ambayo kiasi kikubwa urudi angani baada ya kuevaporate na kingine uishia baharini. Kidogo ulicharge ground water na ardhi. Hii kitu ni mjadala mpana sana.
 
Miradi ya kuvuna maji ipo. Mfano bwawa la mtera.

Tatizo siyo fikra. Tatizo ni PESA
 
Safi Sana kiongoz, kwel kabisa fikra ndio uhuru wetu. Nimekuelewa vzr Sana na nimepata kitu kutoka kwako hongera Sana
 
kutatua tatizo la maji anahitajika mtu mwenye uppendo na anayeumizwa na shida za watu wake. mtu mkatili hawezi mhurumia mama anayeenda 5km kufuata maji.
photo+3.JPG
 
Nimekuelewa ndugu Analogia Malenga. Tunaweza kutumia maji yatokanayo na mafuriko kama sehemu ya vyanzo vyetu vya maji hasa wakati wa kiangazi. Zipo nchi zilizofanikiwa katika hilo na wao hawakusanyi tu maji ya mafuriko bali runoff yoyote inayokuwa generated wakati wa mvua mfano ni Namibia. Upo utaalam unaotakiwa kuwezesha hilo lakini pia fedha kwa ajili ya study ya namna hiyo pamoja na ile ya kujenga miundo mbinu yake. Utayali wa serikali kwenye project za namna hii ungesaidia kwa kiwango kikubwa hasa kwa maeneo kame kama Dodoma lakini pindi yapatapo mvua basi tunashuhudia maji mengi kama runoff na mwisho hutoweka baada ya siku chache na hivyo kutuacha na tatizo lile lile la uhaba wa maji. Maji yanayozalishwa kule kwenye visima vya Mzakwe kamwe hayatakaa yatosheleze mahitaji ya maji kwa mji wa Dodoma na hasa kwa siku za usoni ambapo mji unakua na mahitaji kuongezeka. Alternative source ya maji iliyoandaliwa ni ipi? Zipo techniques za kutumia ili kuweza kufanya flood mapping kwa maeneo yote unayotaka. Na unaweza kwenda mbali kwa kuangalia kiasi cha maji unachoweza kukusanya na hivyo ukafikiria jinsi ya kuhifadhi maji hayo iwapo bado kwa eneo hilo yatasaidia zaidi. Lakini kulingana na uhifadhi wako unaweza kuhifadhi maji hayo mwaka huu yakakusaidia labda kiangazi cha miaka 5 ijayo. Hauyapotezi. Swali ni je serikali yetu ipo tayari kuwekeza kwenye tafiti hizo? Na je ipo tayari kuinvest kwenye project hizo? Au tuendelee kuona mafuriko, tupoteze maisha na mali za watu. Lakini pia tuyapoteze maji hayo ambayo kiasi kikubwa urudi angani baada ya kuevaporate na kingine uishia baharini. Kidogo ulicharge ground water na ardhi. Hii kitu ni mjadala mpana sana.

Pesa! Pesa! Nakuomba mkuu angalia, pesa mabazo raia hutumia wakati wa kiangazi ili kujipatia maji kwa matumizi mbalimbali. Pia angalia bei za maji zitakavyopanda kutokana na kukua kwa demand ya maji kwa sababu ya kukua kwa miji.

Sasa chuku hela mara idadi ya miaka ambayo raia atatafuta maji, then fananisha na hela kidogo ya kufanyia tafiti (Relatively).

Hata kwenye sekta ya uchumi, bahati mbaya hatuna wachumi tuna wabahili tu.
 
Back
Top Bottom