Tatizo la maji Kimara

Tatizo la maji Kimara

mchaga asilia

Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
10
Reaction score
0
Habari ndugu zangu.

Nimevumilia sana ila uvumilivu umefika kikomo.

Mimi ni mkazi wa Kimara suca. Jaman hatujapata maji haya ya DAWASCO unakwenda mwezi wa pili sasa.

Napata mashaka na kujiuliza hivi 'maji sasa imekua ni bidhaa na si huduma tena kama zamani? Je hawa wanaojiita DAWASCO ni akina nani na wanafanya kazi kwa maslahi ya nani?

Wananchi ama wale wenye magari ya kuuza maji?

Ndugu zangu DAWASCO na wananchi wengine kwa mwendo huu tutafika kweli?
 
Mi naishi Kimara Mwisho huu ni mwezi wa4 sijaona bomba likitoa tone la maji....maji ya bomba yakitoka bill inakuja c zaidi ya 10000, lakini kwa sasa nalazimika kutumia zaidi ya Tsh 80000 kwa mwezi
 
Na cha kushangaza sio kwamba Maji hayapo,kila siku wanatoa sababu kuwa mfumo wao wa usambazaji una tatizo,na wala hawalishughuliki.
 
Wenye biashara ya maji kwenye magari Kimara ni madiwani uliza utaambiwa. jengeni visima mvune ya mvua au wapigeni chini madiwani mafisadi mwakani
 
Poleni sana..jaribun kuchimba visima
 
Back
Top Bottom